MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Nipe mstari unaosema Maria alipaa kwenda mbinguni.
 
mtu yeyote akiamini kanisa linatumia biblia lazima atalipinga, maana yaliyopo kwenye biblia na yanayoendelea kwenye kanisa haviendani
ukielewa misimamo ya kanisa na chanzo cha imani yao huwezi ongelea biblia
hawafuati biblia, na ndio maana hawapendi watu wasome biblia. wanaona haina umuhimu
Luther alivoanza kufundisha chuo kikuuu akapata access ya kusoma biblia akashangaa sana, akaona mbona hatufuati biblia. katika kuhoji akaonekana muasi
 
Unazungumzia hiyo karne ya 14, Martin Luther aliikuta Biblia ikiwa na vumbi katika maktaba. pamoja na usomi wake hakuwa kukutana na biblia hata ikitajwa kanisani au popote. Hiyo ndivyo ilivyokuwa Kanisa la Roma, ilikuwa inaelekea kuwa dola zaidi ya Kanisa. Uasi wa Martin LUther ndio iliyofanya Kanisa la katoliki kurudi nyuma na kuanza tena kutumia Biblia
 
Alipalizwa hakupaaa
ingekuwa vyema kama ungemrekebisha kama ulivyo sema hapo huku unamuonesha na huo mstari unaosema kuwa alipalizwa ili kusupport jibu lako hvyo ndivyo mkristo hutakiwa kujibu maswali ya kiimani
 
Luther alivoanza kufundisha chuo kikuuu akapata access ya kusoma biblia akashangaa sana, akaona mbona hatufuati biblia. katika kuhoji akaonekana muasi
Yameulizwa maswali mawili, kwanini aliachana na kanisa katoliki na kwanini alinyofoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia?

Umejibu swali la kwanza, kujiondoa kwake kwenye ukatoliki. Swali la kwanini alinyofoa baadhi ya vitabu halijajibiwa.
 
uongo wa mchana hebu lete andiko.
maana maria ndiye aliyesema hivyo.
LUKA 1:46-48.
anasema watamwita mmbarikiwa lakini sio Mungu kusema tutamwita hivyo
Neno la MUNGU halijipingi unataka kudhihirisha kua unasema uongo
Haraka zako za kuambiwa zinakuelekeza siko
Ludi nyuma katika enjili hiyo ya Luka 1:41 roho mtakatifu anamjaza Elizabeth na kunena kua Mariam amebarikiwa kuliko wanawake wote hayo maneno yalinenwa na Elizabeth Kwa njia ya roho mtakatifu siyo Mariam
Luka 1:43 Elizabeth anakiri kua Mariam ni mama wa BWANA wake (MUNGU) kwako hiyo anafanywa kua baraka rejea mwanzo 12 :2-3
Kama alivyo muandaa Ibrahim na uzao wake kua baraka unakamilishwa Kwa mwana mwali Mariam
Usichoke kusoma biblia katika kitabu cha mwanzo 3:6 mwanamke anachuma dhambi na kumpa adamu tunda la dhambi wote wanaanguka dhambini na hayo Mwanamke anasababisha
Mwanzo 3:15 Lakini MUNGU ana ahidi ukombozi Kwa mwanamke kua uzao wake utamshinda shetani na ushawishi wa kutenda dhambi
Katika yeye ukombozi unakuja dhambi ililetwa na mwanamke mwa 3 :6 na mwana wa mwanamke Mariam Luka 1:43 anaukomboa ulimwengu
Huyo Mwanamke ndiye analeta baraka za Ibrahim Baba yake dunia yote inabarikiwa mwanzo 13:2-3
Yesu Kristo akizaliwa na mariamu si kibailojia wala hakua na Baba wa kibailojia MUNGU alichagua MTU Bora kuliko wote kwakwe yeye aweze kuufikia ulimwengu ulio potoka uwezo kumludia yeye muumba wake
 
Yameulizwa maswali mawili, kwanini aliachana na kanisa katoliki na kwanini alinyofoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia?

Umejibu swali la kwanza, kujiondoa kwake kwenye ukatoliki. Swali la kwanini alinyofoa baadhi ya vitabu halijajibiwa.
sijawahi kusoma popote juu ya kwamba huyo jamaa aliondoa vitabu kwenye biblia
na sidhani kama vitabu vilivyotolewa na havikujumuishwa kwenye biblia ni kitu kilifanywa na mtu mmoja
ni wataalam walivisoma wakaona maudhui yake yana walakini. wakavitoa
 
Nenda katafute vitabu vilivyotolewa kisha soma uone kilichomo ndipo utajua haujui.
 
Haujawahi kuombewa?
 
HHakufa alipalizwa mbinguni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…