Mjadala maalum wa Afya ya Akili-Msongo wa Mawazo, Hasira na Hofu

Mjadala maalum wa Afya ya Akili-Msongo wa Mawazo, Hasira na Hofu

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,973
Reaction score
6,750
Habari za wati huu;

Leo nimeona nilete mjadala kidgo ili tujadili kuhusu afya ya akili na upatikanaji wa huduma rafiki za afya ya akili(Mental health services)Kwa Tanzania

Nitaanza kwa kufafanua tafsiri ndogo inayohusu afya ya akili-Afya ya akili inahusiana zaidi na hali ya kiakili/ubongo ya mwanadamu ambayo inawezesha mtu kuweza kuishi maisha yake kawaida na kushirkiana na wanajamii wengine vizuri.Ni ili hali ya mtu kuwa na uhusiano mzuri wa kihisia yeye binafsi pamoja na wale wanaomzunguka.Mtu mwenye matatizo ya akili anakuwa na matatizo kwenye mfumo wake wa akili,ubongo na hata wakati mwingine huathiri uwezo wake wa kimwili(physiological)

Afya yenye akili hupelekea mwili wote kuwa na akili na Mwili wenye afya hupelekea pia akili yenye afya na zaidi jamii yenye afya hujenga wanajamii wenye afya.

Kwa kuwa lengo langu ni kuchokoza mjadala basi tujadili hapa kuhusu uelewa wa watu kuhusu afya ya akili,tiba na upatikanaji wa huduma rafiki kwa watu wenye matatizo ya akili.Tunaweza pia kujadili chanzo na visababishi vya matatizo ya akili katika jamii zetu na namna tunaweza punguza madhara yake


Karibuni
 
Maktari na wananchi wanapokutana na watu wenye kupitia mitihani ya mfululizo wawaekeze kuwaona madaktari wa akili na kisaikolojia.
 
Awareness kubwa inahitajika kuhusu tatizo hilo watu hawajui kama ni tatizo na kwamba kuna na maktari wa kuwahudumia kabla tatizo halijakuwa kubwa
 
Halafu watoto wa siku hizi mbona siyo kama zamani yaani uwezo wa kufikiri ni mdogo, hata akikaa sehem akiwa peke yake ukamchunguza unaona utofauti. Huwa nawaza upande wa hizi chanjo huenda zikachangia pakubwa.
 
Halafu watoto wa siku hizi mbona siyo kama zamani yaani uwezo wa kufikiri ni mdogo, hata akikaa sehem akiwa peke yake ukamchunguza unaona utofauti.
Huwa nawaza upande wa hizi chanjo huenda zikachangia pakubwa


Mfumo wa malezi pia unachangia sana!
Wazazi wa siku hizi hawafundishi watoto kujitegemea hata ktk kujifunza kujifanyia mambo madogo madogo.

Mtoto anakula mezani sahani aje kuondoa dada wa kazi?!

Mtoto anafuliwa nguo na yaya ?!

Kila kitu anafanya yaya Eti wazazi wanaona ndiyo kuwapenda watoto wao !
 
Mfumo wa malezi pia unachangia sana!
Wazazi wa siku hizi hawafundishi watoto kujitegemea hata ktk kujifunza kujifanyia mambo madogo madogo.

Mtoto anakula mezani sahani aje kuondoa dada wa kazi?!

Mtoto anafuliwa nguo na yaya ?!

Kila kitu anafanya yaya Eti wazazi wanaona ndiyo kuwapenda watoto wao !
Mfumo wa malezi pia unachangia sana!
Wazazi wa siku hizi hawafundishi watoto kujitegemea hata ktk kujifunza kujifanyia mambo madogo madogo.

Mtoto anakula mezani sahani aje kuondoa dada wa kazi?!

Mtoto anafuliwa nguo na yaya ?!

Kila kitu anafanya yaya Eti wazazi wanaona ndiyo kuwapenda watoto wao !
Hapa kipengele cha malezi inatakiwa wazazi wabadili mtazamo la sivyo kizazi shupavu tutakuwa tunakisoma kwenye kumbkumb za kihistoria
 
Tunapozungumzia afya ya akili lazima tuzungumzie ubongo,kwasababu akili ni sehemu ya ubongo.

...kiukweli ubongo ndo sehemu nyeti Sana na iliyobeba Siri kubwa ya maisha ya mwanadamu...

Ubongo umebeba hisia zote na akili zote, ubongo ndo umekusanya mifereji yote ya milango ya Fahamu...ubongo ndo sehemu iliyobeba kumbukumbu zote za mwanadamu,naweza nikasema ubongo ndo master engine ya mwanadamu..

...Afya ya ubongo inapokuwa nzuri bila shaka na afya ya mwili pia hua nzuri.....ubungo unaposetiwa vizuri hutoa matunda mazuri,pia unaposetiwa vibaya hutoa matunda mabaya..

Wataalamu wanasema vita ya kiakili ni mbaya zaidi ya vta ya mtutu.....kuna watu wanaweza wakakuadhibu kupitia ubongo wako ....pia unaweza kuendeshwa kupitia ubongo wako.

Vijana wengi huaribu future zao kwa kuharibu bongo zao... either kwa kutumia madawa ya kulevya,au kuigaiga mambo ovyo/kufuata kila wanchokisikia au kukiona,kuruhusu maneno hasi kutawala maisha yao...pia kushindwa kuzingatia afya za bongo zao.

Ubongo unahitaji kutunzwa kama ulivyo mwili..
Tunaupenda mwili wetu kwasababu ndo unatufanya tunaonekana,hvyo tutaoga Safi,tutaupaka mafuta mazuri,tutaupulizia marashi mazuri bila kusahau diets na mazoezi ya apa na pale ili tu tuonekane vizuri...

Lakini cha kusikitisha tunasahau afya ya ubongo wetu..ubongo nao unahitajia Sana kufanywa hayo yanayofanyiwa mwili,kuoshwa,kupakwa mafuta,kulishwa chakula kizuri na kuufanyisha mazoezi mazuri..
------------------------------------------------------------
...tunapozungumzia ubongo tunazungumzia vtu vingi sana,lakini vtu vyote hvyo vmejumuishwa na kugawanywa ktk utendaji wa aina mbili.

1:- kuna upande unaoratibu matendo ya hiyari (conscious mind),mfano..kuandika,kutembea,kunyoosha mkono n.k

Hii sehemu ya ubongo ni sehemu ya kwanza inayopokea matendo yote tunayoyafanya kwa mara ya kwanza hasa ktk kujifunza ktu..mfano,unapo jifunza kuendesha gari.

Sifa ya hii sehemu ipo limited na inafanya kazi pale tu inapoitajika kufanya kazi...ndomana ktk kujifunza ktu huwa tunatofautiana muda wa kukielewa hcho kitu.ii

Pia hii sehemu naweza ifananisha na application software ktk computer na ubongo ndo software.

2:-kuna upande unaoratibu matendo yasio ya hiyari (subconscious mind)..mfano,kupumua,mapogo ya moyo,kulala n.k

Hii ni sehemu nyeti ambayo imebeba Siri na nguvu kubwa...mbali na hzo kazi apo juu nilizozitaja hii sehemu ndo maisha ya mwanadamu yapo apo.

Mitume,na watu wote waligundua vtu au waliofanya makubwa ktk ulimwengu huu,ni kutokana na kufunuliwa au kutumika kwa sehemu hyo.

Mambo yote anayoongelea mshana sijui kutoka nje ya mwili,hii ndo sehemu pekee inayo operate hayo mambo.

Hii sehemu ni kama shamba ambapo inapokea kila unalolingiza (mbegu/mawazo) na kuactivate kuwa kweli katka maisha yako.
(A man become what he thinks about most of time)

Sifa ya hii sehemu unlimited na hutenda kazi masaa 24 kwa sku kupumzka kwake labda mtu afe.

Apa ndo afya ya akili inapokuwa...stress zote huku ndo zinapozaliwa,chuki,furaha,mapenzi,huzuni ndo uku zinapoanzia.

Ndomana kuna muda yale maumivu ya mapenzi yanapotokea hasa kuachwa,huwa moyo unauma kweli...tatzo sio moyo Ila yale maumivu yanatokea uku na unapoweza kuactivate na kucontrol hii sehemu Basi wewe maumivu ya kuachwa kwako hayatokugusa kabsa...😅😃

Hii sehemu naweza ifananisha na system software ktk computer.

Mambo ya brainwashed yanafanyika uku,wale wavutaji bangi maajabu mnayoyaona hutokea uku,wale walevi pia.

Our greatest power is our capacity to choose.... suggestions and comments of others have no power to hurt you.

APO NIMEANDIKA KWA KIFUPI SANA,KIKUBWA TULINDE AFYA ZETU ZA AKILI KWA MAFANIKIO YETU NA KIZAZI CHETU.
 
Asante kwa darasa zuri.

Nimependa hiyo paragraph ya last but one, nikikunukuu , “our greatest power is capacity to choose “

Hiyo inamaana gani? Naomba fafanua tuelewe zaidi.

Je mtu anayepitia jambo gumu anaweza kuchagua kutoumizwa na hilo jambo?

Au inawezekanaje kwa mfano?

CC : King Sae
 
Mada nzuri lakini serekali ilitakiwa iongeze wataalam wa afya ya akili ikiwezekana kuwe na mtaalam mmoja kila kata wenzetu wanalichukulia umuhimu mkubwa hili jambo mfano magerezan wapo wengi mtu anabaka mbuzi badala Hakimu ampeleke hospatal anamfunga.
 
Back
Top Bottom