Mjadala: Mafanikio gani yametokea baada ya Sensa ya 2012?

Mjadala: Mafanikio gani yametokea baada ya Sensa ya 2012?

Mwanakwetuuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2022
Posts
1,011
Reaction score
2,283
Wakuu Rais ametangaza Sensa mwaka huu itafanyika mwezi wa nane,mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2012 .Je kuna mafanikio gani yaliyotokea Kwa kuhesabu Sensa ya mwaka 2012? Lakini pia mwaka 1988 ilifanyika Sensa ya watu na makazi baadae ikafanyika mwaka 2002 , katika vipindi hivyo vyote vya kufanya Sensa kuna faida zipi ?Tusemezane@Nguruvi3
 
Itawezekana kusema kwamba, kwa sasa Tanzania INA idadi ya watu kadhaa usipojitokeza kuhesabiwa,.?

Hiyo ndiyo faida mkuu!

Unalingine.?
 
sensa ya watu na maendeleo
uwezi weka kipaumbele budget ya hospitali kubwa sehemu yenye watu 10 ukaacha 800 hao wapewe zahanati
 
Sensa inawasaidia wazungu kujua nchi yetu ina watu maskini wangapi wanaokufa njaa huku viongozi wetu wakihubiri uchumi unapaa kama "the wings of Kilimanjaro" and "Royo Tua" ila msaada wao unaangalia maslahi yao kwanza!!

Sensa za nyuma pia zilikagua waumini wa kila dini wako wangapi nchini ili kuwanyima fursa za elimu ya juu na kazi waislamu, una jingine?
 
Hata nyumbani kabla ya kupika chakula huwa wanauliza, wako wangapi.

Mzee kabla hajalipa ada, anahesabu watoto wake, anagawa kwa kipato chake.
 
Back
Top Bottom