MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

hii kitu nataka kujaribu
 
Naomba kujua gharama za kukodi shamba , kulima mpka kuvuna na inachukua muda gani ili mpunga kuwa tayari kwa kuvunwa na ekari 1 inatoa gunia ngapi
 
Karibu Morogoro ulime!! Roughly kwa eka moja unahitaji la 6-8 kukodi adi kuvuna. Eka 1 waweza pata gunia 20-40.
 
Karibu Morogoro ulime!! Roughly kwa eka moja unahitaji la 6-8 kukodi adi kuvuna. Eka 1 waweza pata gunia 20-40.
Hivi mtu akikuandikia wewe hivi utaelewa anamaanisha nini??
 
Too General mkuu, labda ingekua je analima nje ya mashamba ya umwagiliaji au ndani ya mashamba ya umwagiliaji
Karibu Morogoro ulime!! Roughly kwa eka moja unahitaji la 6-8 kukodi adi kuvuna. Eka 1 waweza pata gunia 20-40.
 
Niko hapa kujua hiyo mbegu inayotoa gunia 40 kwa heka. Kukodi heka huku geita ni laki mbili gunia 17hadi 20 hapo ujipange kwa palizi
 
Nipo moshi lower
Kukodi shamba mita mia laki tatu,
Kuhudumia shamba hadi mavuno wastani kama laki 7-8 hivi
Kwa mbegu za huku ni saro 5 na 64 huwa ni muda wa miezi mitatu hadi minne mpaka mavuno..
Kwa mita mia waweza pata gunia 17 hadi ishirini
 
Hii ndio matumizi sahihi ya jamii forum. Tumeshapata taarifa ya fursa ya kilimo cha mpunga karibia kila pembe ya Tanzania. Bado KATAVI ili kabla ya kuingia kwenye ujasiriamali huo kichwa kichwa uwe umetathmini pro and cons, usije ukaingia kichwa kichwa kama ufugaji wa kware na sungura. Hongera uliyeanzisha uzi
 
Habari wadau, natarajia kulima mpunga msimu wa masika, lakini kabla hujaingia LAZIMA ufanye udadis ili kujiridhisha!

Ukiwauliza wakulima wenyewe wanakuambia heka moja inatoa magunia 20-30
Wengine magunia 15-20

Sasa UPI ukweli?

Naomba mwenye maelezo ya kina, kama inawezekana anieleze ni aina gani ya mbegu ya mpunga inayovumilia hali ya hewa na yenye mavuno mengi /mazuri!

Naomba kuwasilisha wakuu!

Karibuni nyote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanakwambia tu kuwa heka moja inatoa gunia hizo. Ila awazungumzii changamoto.

Wenzio waliingia kama wewe wakaishia kutukana.

Field research ni muhimu sana. Plus pokea informations zote, na sio kutaka kujua utavuna kiasi gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inafwatana na sehemu unayolima pia upatikanaji wa mvua mimi nilivuna 23 gunia kwa heka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nililima msimu wa 2017/18 na msimu huu 2018/19 nitalima tena.

Msimu uliopita, nililima ekari sita (06). Kati ya hizo, ekari tatu (03) nilipanda mbegu iitwayo super mkombozi ambayo hutumia siku 90 shambani tangu kupanda hadi kuvuna..na ekari tatu (03) nyingine, nilipanda mbegu aina ya Sarro ambayo hutumia siku 120.

Matokeo:-

Kwa ekari nilizopanda super mkombozi, nilivuna wastani wa magunia 17 Kwa kila ekari. Na Kwa zile ekari nilizopanda sarro, nilivuna wastani wa magunia 25 Kwa kila ekari. SIKUTUMIA MBOLEA HATA ROBO KILO

Changamoto:-
Kutegemea mvua ni changamoto kubwa. Mavuno yaliathiriwa na ukame wa takribani siku 24.

Changamoto nyingine, ni umbali. Mimi nipo mjini na pia ni mwajiriwa. Kutegemea mtu mwingine akukodie shamba, akulimie na kazi zote za shamba akufanyie yeye..LABDA AWE MALAIKA. ILA MSIMU HUU NALIMA TENA
 
Kaka umelima wap....
Hata mim nlilima msimu wa 2017/2018 ila mwenzangu una nafuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuja pm mkuu tuyajenge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…