Mi ningemshauri mtu yeyote anayetaka kuanzisha mradi wowote asianzishe kwa majaribio au kama part time inayokosa proper concentration, vinginevyo ataishia kukiri kutofaidika na mardi na kisha kutoa mchango hasi juu ya mradi huo.
Naona walio wengi katika Jf wanataka kufanyia kazi habari za kusikia sikia tu bila kuzifanyia upembuzi yakinifu yaani kujishughulisha kwa kina kujua kila kitu kuhusu mradi.
Kwa Ifakara, Mang'ula, Kiberege, Mkula nk, ni bora mjasiriamali wa kuja akanunua mchele na kuuza mbali badala ya kulima mpunga. Katika kipindi cha mavuno, yaani june,julai mpaka August watu huvuna mpunga na kuuza kwa bei ndogo sana, hasa sehemu za Chita, Mngeta na Mlimba, na kisha mchele huohuo huuzwa kwa bei karibia mara tatu yake baada ya muda mfupi wa miezi mitatu tu yaani November,december mpaka march.
Sasa mdau, kama kweli unataka kukwepa adha ya kulima mpunga,na kupata faida ya muda mfupi fanya kununua mchele badala ya kulima mpunga. kule ni bondeni, kuna mito mingi which means pia kuna malaria nk, mdau kash kash hizo baba utazimudu?
Halafu kuna vishawishi vya ndogondogo kama alivyosema mdau hapo juu, si utamalizia mtaji huko? Naomba ufikirie mara mbili mdau kabla hujaamua!