IslamTZ
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 309
- 182
Tumesikia malalamiko memgi juu ya baraza jipya la mawaziri la Rais Samia.
1. Je Rais na mamlaka nyingine za uteuzi zizingatie uwiano wa makundi au la?
2. Pili, mamlaka zizingatie uwiano wa makundi ya aina gani? Jinsia, rika, dini, kanda, kabila nk?
3. Hali ikoje baraza hili na nini kifanyike?
Nimemsikia Godbless Lema akikosoa mambo ya kuangalia uwiano, amnbapo alitaka weledi tu uzingatiwe? Je iwe hivyo? Wakati tukijadili haya, tukumbuke kuwa wenzetu wa Kenya na baadhi ya nchi nyingine za jirani ni matakwa ya katiba uteuzi uzingatie sura ya kitaifa, ambao ndio huo uwiano? Nasi tufuate msingi huo? Au tupuuzie tu?
Karibuni
- Kuna malalamiko ya kukosekana usawa wa jinsia, mawazir wanawake ni 36% na manaibu ni 20 tu
- Kuna malalamiko ya kanda fulani kupendelewa, kama mkoa wa Pwani kuwa na mawaziri (na maanaibu) 5
- Kuna malalamiko kuwa walioachwa wote ni Wakristo, ingawa kwa upande mwingine hivi sasa mawaziri na manaibu Wakristo ni 32 ukilinganisha na Waislamu 18 tu.
- Pia yapo malalamiko kuwa watoto wa familia za viongozi wameendelea kuingizwa kwenye baraza, kama yalivyowasilishwa na Malisa GJ na Thabit Jacob aliyewataja kabisa watoto hao kuwa ni Nape Nnauye, Januari Makamba, Pinda, Mavunde, Ndejembi.