Mjadala: Muziki sio Haramu. Inategemea na uimbaji wake

Unajua unacho kiandika na unarejea kwenye nini ?

Kwami vipasa sauti ni sharti la kukubaliwa ibada ya mtu ?

Nakuuliza tena unakijua unachokijadili ?


Mkuu mambo haya yanahitaji uelewa mdogo tuu.

Sio kila kitu kilichotumika zamani kwenye dini kitumike sasa hivi.

Muhimu ni zile amri za MUNGU ambazo ndio amri za Asili za ulimwengu.
 
...Hata huo muziki wa Qaswida au injili ukiimbwa kilabuni ni haramu Kwa sababu umeimbwa sehemu isiyosahihi.
Labda hiyo qaswida maana siijui na siwezi kuisemea, lakini muziki wa injili ni halali kuimbwa popote hata kilabuni
 
MPAGANI MKUBWA WEWE. KWAMBA DUNIANI NDIO KWETU WANADAMU! HIVI KWELI WEWE NI MKRISTO UNAYESOMA BIBLIA? UA NYINYI NDIYO WALE WA MISALE NA LITURGIA!
KUNA NYIMBO HATA MIDUNDO YA MUZIKI HAIMPI BWANA YESU KRISTO UTUKUFU. NI CHUKIZO. UNAJUA NYINYI WAKRISTO TANGU MLIPOAMUA KUMWASI ROHO MTAKATIFU AKAWAACHA, MUMEBAKI MNATUMIA AKILI ZENU ZISIZOFAA KUMWABUDU MUNGU.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Unamaanisha nini mkuu kusema hivi ?
 
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 



😀😀😀😀

Kwenu ni wapi Sheikhe???

Wewe ni mavumbi na mavumbi utarejea.

Hii dunia mnaikana Kwa sababu mumeiharibu 😀😀😀

Embu nijulishe kwenu wapi?
 
Unajua unacho kiandika na unarejea kwenye nini ?

Kwami vipasa sauti ni sharti la kukubaliwa ibada ya mtu ?

Nakuuliza tena unakijua unachokijadili ?
Sirejei kwenye kitu

Sijaelewa ulicho kiandika
 
Unamaanisha nini mkuu kusema hivi ?
Watu wamekua wakiishi kwa kuangalia kila kitu walichofanya hao manabii wa kale wakiamini kila kinachoenda kinyume na hapo basi ni dhambi
 
Watu wamekua wakiishi kwa kuangalia kila kitu walichofanya hao manabii wa kale wakiamini kila kinachoenda kinyume na hapo basi ni dhambi
Kwa namna fulani nakubaliana na wewe.

Japokuwa yako mengi watu wanayasema kwamba ni maamrisho ya manabii lakini uhalisia wake ni maamrisho ya ufahamu wao.

Kwa kiasi fulani nakubali usemacho.
 
Si kila halali kwako iwe halali kwa wote, na si kila haramu kwako iwe haramu kwa wote.
Kwetu muziki ni haramu, itabakia kuwa haramu mpaka siku ya mwisho.
kuna wanaofuata matamanio ya nafsi zao, wakatumia mikono yao (KUANDIKA) na vinywa vyao ((KUHUBIRI) wakahalalisha iliyo haramishwa na wakaharamisha iliyohalalishwa hawa ni waovu kupikndukia.
 


Nipe Aya ya Qurani iliyoharamisha muziki.

Usinipe hadithi za mtume Muhammad na Mswahaba wake. Hayo tunahachukulia Kama maoni ya Waandishi au manabii na mitume ambao ni Binadamu Kama Sisi tuu
 
Mkuu unaweza kunipa marejeo katika uislamu yakielezea nini maana ya muziki ?
 
-Mwanzilishi wa Muziki ni Mungu mwenyewe
-Musiki ulikusudiwa kwa ajili ya Ibada
-Lusifa kabla ya kuasi ndie aliyeumbwa na aina za vyombo vya musiki (Ezekiel 28:13)
-Lusifa alipoasi amegeuza matumizi ya asili ya Musiki wa Ibada kwa mwenyezi Mungu
uwe kwa ajili ya ibada zake

Nguvu ya Muziki
-Musiki unaweza kufukuza mashetani au kukaribisha mashetani
-Musiki wa kimbingu hufukuza mashetani (kumbuka kisa cha sauli kutoka mapepo kwa -muziki tu)
-Musiki unaweza kualika uwepo wa Mungu katika Ibada
-Musiki unaweza kualika uwepo wa mashetani katika ibada (angalia ngoma za mashetani za tanga/pwani zinavyopigwa watu hushikwa na mapepo.
-Musiki unaweza kufanya uue
-Musiki unaweza kukufanya uzini hata kama hukuwa na lengo
-Musiki unaweza kukufanya kumchagua mtu kwenye cheo hata kama hukunia
-Musiki unaweza kukufanya ununue bidhaa fulani hata kama hukudhamiria (ndio maana matangazo ya TV radio huanza na musiki)
Kwa ujumla Muziki huweza kuteka maamuzi yako

13 "Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari." Ezekiel 28:13

-Musiki wa Ibada za Mwenyezi Mungu na Za shetani hutofautiana kwa namna tu unavyopigwa.
1.Mapigo 3/4 na 4/4 ndio mapigo ambayo huendana na mapigo ya moyo na huu ndio muziki ambao haupagawishi.
2. Ukitaka mtu ambaye hachezi musiki acheze ongeza kati ya mapigo kwa kadiri kasi inavyozidi ndivyo kupagawa huzidi basi hapa ndipo ibada huchafuka na kuwa makelele na mazingira hayo ndio rafiki kwa shetani.

Singeli na kupagawa
1.Katika miondoko ya singeli kasi ya vyombo inavyozidi ndivyo kupagawa huongezeka
na wanawake huvua nguo.(kinachofanyika hapa ni kuchanganya vyombo vingi na kuongeza kasi ya mapigo)
2.Kasi ya mapigo ya musiki katika nyimbo za ibada ndio sababu kubwa ya kupagawa katika ibada na hii ndio asili ya makanisa ya wamarekani weusi, ambao tumeiga makanisa yao.
na huu hudhaniwa ni utendaji wa roho mtakatifu.

Nukuu "Nioneshe musiki wa taifa lako, nitakuambia maadili ya taifa lako"
 
Soma kitabu cha wimbo uliobora utaona muziki wa kidunia aliouimba Suleiman.

Daudi yeye alicheza muziki mpaka akavua nguo.

Zipo sherehe nyingi Sana ambazo muziki ulipigwa
Naomba niulize swali? Daudi pia alizini kwa hivyo kuzini ni halali?. Kwa sababu daudi kafanya Jambo baya haihalalishi Hilo Jambo kuwa zuri. Ndio maana tumetakiwa tufanye Yale mapenzi ya Mungu pekee. Jambo unalofanya jiulize je hili Jambo linampendeza Mungu? Kama halimpendezi Mungu liache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…