MJADALA: Ni changamoto gani unakumbana nayo kwa kuchelewa kuoa/kuolewa?

MJADALA: Ni changamoto gani unakumbana nayo kwa kuchelewa kuoa/kuolewa?

Kwa tamaduni na mazingira ya kiafrika yalivyo ukishafika miaka 33+ ni vigumu sana kupata mwenza aliye sahihi hii ni kwa jinsia zote!

Kwa umri huo watu wa umri wako ambao wako available watakuwa ni wataraka au masingle mothers/fathers na waliokobuhu kwenye mahusiano kiasi kwamba hata kuumiza au kuumizwa hawaoni shida kabisa.

kiufupi wengi umri huo wanakuwa makapi, cream zishawahiwa
 
Please, naomba unisamehe......kusema kweli nilisema kwa masihara tu,sikujua kama nitakuumiza kiasi hiki. Nimekosa amani kuona nimekukwaza rafiki yangu.
Hapa nimekuelewa yameisha

Kiukweli nilihisi limekutoka moyoni japo utani ila mwanaume kuitwa mmbea haipendezi nashukulu kama umetengua kauli.
 
Habari za jumatatu,

Ni changamoto gani unazipata katika harakati za kutafuta mke kama wewe ni wale waliochelewa kuoa. Kwa mtazamo wa jamii zetu za kiTz mwanaume au mwanamke aliezidi miaka 35 hajaoa au kuolewa ni kuwa amechelewa. Hii sio sheria mwingine anaweza kuwa na mtazamo tofauti.

Mimi binafsi changamoto ninazopata ni hizi;

1.Umri-wanawake wengi kwenye jamii zetu ambao hawajaolewa umri wao ni 22-26. Kwangu mimi bado wadogo yaani tofauti ya umri naiona kubwa.

2.Siko tayari kuoa mwanamke mwenye mtoto-naomba nisieleweke vibaya, huu ni msimamo tu nimeamua hivyo. Changamoto kubwa sasa ni kuwa wale ambao naona ndio umri sahihi wa kuolewa na mimi wengi wao wana mtoto/watoto.

3.Nachagua sana (Naambiwa hivyo inabidi nikubali)-kuoa bila kuchagua inawezekana kweli? Huyu ni mtu nitakaekuwa nae kwa maisha yangu yote sasa inabidi nipate mtu nilieridhika nae.

Tuchangie thread hii kwa lengo la kusaidiana, kurekebisha na kushauri.
Hahaa nimecheka eti 'nachagua sana' hakuna ubaya kwenye kuchagua sana maana mtu ambae utaishi nae maisha yako yote ni lazima roho yako iwe imeridhika la sivyo ndoa itakuwa ndoano, lakini unatakiwa ujue no one is perfect na huyo utakayemuona umeridhishwa nae anaweza asiwe ameridhishwa na wewe
 
mbona wapo wengi mkuu wa 27-34 ambao hawajaolewa na hawana watoto kama uchaguzi wako ulivyo.
kuchagua sana sio tatizo, tatizo ni kuchagua bila kuwa na standards, weka viwango vyako vilivyohalisi chagua mwenye afadhali.
Maisha hwyasubiri, wengi huoa nusu wakqmilifu kama wao walivyo nusu wakamilifu. hizo nusu mbili ndio zinafanya ndoa kamilifu mkuu.

ila hata hao uliowwtaja kama wadogo sana ukikuta kaivishwa vizuri na wazazi ni bora sana tena saana
Umemshauri vizuri sana pacha wangu
 
Nimependa ushauri wako
 
Back
Top Bottom