Gamba la Mbu
Senior Member
- Jun 28, 2020
- 159
- 419
Wakuu salaam!
Agosti 12, 2020 ilikuwa ni siku ya Vijana Kimataifa. Tanzania kama ilivyo kwa Nchi zingine kote ulimwenguni iliazimisha siku hii kwa kutambua uwepo wa vijana katika ujenzi wa taifa.
Kwa huzuni kubwa siku hii ya vijana imeazimishwa huku ikishuhudia vijana wengi wa Tanzania wakiwa wamegubikwa na sononi na khofu kubwa ya mustakabali wa maisha yao kwani japo idadi ya Vijana ni kubwa lakini vijana wengi wamekwamishwa kuingizwa katika ushiriki wa ujenzi wa nchi yao kwa kunyimwa ajira kwa takribani miaka 5 iliyopita. Yaani tangu 2015 - 2020.
Kumbuka vijana hawa ndio warithi tegemewa wa uendeshaji wa nchi siku za usoni. Ndio nguvu kazi ya taifa na bado wana ari ya kutumika katika nyanja zote za kiuchumi.
Uhitaji wa kuanzisha familia na kusaidia familia zao ni kitu ambacho wamekikosa kwa muda mrefu. Ongezeko la single mothers iwe ni indicator moja wapo ya kukosekana kwa fursa za kiuchumi kwa vijana wengi hivyo wanaume kushindwa kuanzisha familia.
Nilitegemea serikali yetu itatoa mustakabali wa uelekeo wa fursa za kiuchumi kwa vijana kwa miaka 5 ijayo ili tupate matumaini mapya.
Lakini imekuwa kinyume chake.
Vijana Wajiari
Hii imekuwa ni kauli inayolazimisha maji kupanda mlima kwa muda mrefu.
Je!
01. Ni nani asiyetaka kujiajiri?
02. Ni nani asiyetaka kuijenga nchi yake?
03. Kwanini serikali itubague kwa maksudi?
04. Mbona kuna upungufu wa kiutendaji katika maeneo mengi ya kiutumishi lakini serikali imegoma kuongeza watumishi?
Ni nini hatma ya Kijana wa Kitanzania kufikia 2025?