Alvajumaa
JF-Expert Member
- Jul 5, 2018
- 5,039
- 6,253
Wakuu
Huku ligi yetu pendwa ya TPL ikielekea ukingoni tunajua kwamba Simba ambaye ni bingwa msimu uliopita atacheza na timu ya sevilla kutoka nchini uhispania,
Nabaki kujiuliza TFF walitumia kigezo gani kuteua timu ya Simba icheze na sevilla?
Nakumbuka walitoa maelezo kwamba Simba alifanya vizuri michuano ya sportpesa ndio maana akapewa nafasi ya kucheza mechi hiyo
Binafsi hii sababu yao sikuona kwamba ina mashiko, ingawa tunajua kwamba Simba msimu huu wako on fire, timu yao ni nzuri ila taratibu zilizotumika kuteua timu zina walakini....
Kikawaida timu za ulaya mfano Real Madrid, Barcelona, Manchester United & City , Liverpool , Chelsea, Arsenal na nyinginezo hua zinakua na "tour" ya mechi za kirafiki,
Mfano wanaweza kwenda Bangkok huku Thailand ili kupata mashabiki na kuuza jezi lakini wakicheza mechi za kirafiki timu za ligi hua wanatoa timu moja ya msimu, yaan wale waliofanya vizuri huchaguliwa na kuunda timu moja ambayo hucheza mechi husika,
Hivyo ukijaribu kuangalia TPL msimu huu tunajua kuna wachezaji wengi wameng'ara na hawako Simba, rejea list ya wafungaji bora msimu huu au angalia takwimu za pasi za mwisho, au angalia nani amechukua mchezaji bora wa mwezi mara nyingi msimu huu
Huu ni uthibitisho kwamba wapo wachezaji wengine ambao walipaswa kupata hii fursa ya kuwakabili mabingwa mara 5 wa michuano ya Ueropa, ila kutokana na TFF kutozingatia weledi basi wakatoa zawadi kwa Simba,
Ieleweke siichukii Simba ila namna ilivyopewa nafsi ya kucheza na sevilla kuna walakini, ilibidi iteuliwe timu ya msimu na kocha bora then wacheze hiyo mechi
Hebu njoo tujadiliane, nini maoni yako juu ya jambo hili?