let us think globally but act locally
Tuwe na elimu inayozingatia utu wa mwanadamu
mbona tumekuwa watu wa maneno bila vitendo
anakumbusha walivyofukuzwa chuo kwa kupinga upuuzi
anasema ukweli unauma lakini ni wa mungu
anatambua waliomfundisha kabla hajatimuliwa chuo
anasema hata ninyi wahadhiri hali yenu ni taabani.
anazungumzia GDP tunayoweka katika elimu, bunge iweke trillioni 3.3 katika bajeti ya elimu. tuweke 10% ya pato la nchi katika elimu
tuwekeze kwenye mfumo wa elimu, tuhakikishe usawa katika elimu kama alivyosema prof mkenda. tuwe na elimu inayojenga uzalendo, tanzania tuwe kioo cha afrika. tuheshimu taaluma za watu, pamoja tutashinda.
amemaliza
anachangia frank massawe. anasema elimu ya nchi tumeharibu wenyewe. tulikosea kuharibu elimu ya mwingereza. sio sawa kusoma kwa kiswahili, dunia ya sasa hivi inatumia kiingereza, tanzania sio kisiwa.
kwa nini tuliua darasa la nane? UPE ilikuwa ni useless primary education
turudishe mfumo wa 4 4 2 2
anachangia mkulima, anasema kwa kweli hali ni mbaya. baba wataifa hakupenda kusikiasikia, bali alipenda kujua na kuona.
tuache kulalamika bila kwenda field kuona hali halisi