Mjadala wa Elimu Live Nkhrumah leo

Mjadala wa Elimu Live Nkhrumah leo

let us think globally but act locally
Tuwe na elimu inayozingatia utu wa mwanadamu
mbona tumekuwa watu wa maneno bila vitendo
anakumbusha walivyofukuzwa chuo kwa kupinga upuuzi
anasema ukweli unauma lakini ni wa mungu
anatambua waliomfundisha kabla hajatimuliwa chuo
 
anasema kwa sasa kielimu tuko kwenye janga
tuweke itikadi pembeni tutafute suluhu
 
tunasema sana lakini mabeberu world bank na imf wanatuamulia. hatuwezi kuamua wenyewe? tuamue kuzingatia nuru au giza?
 
anapendekeza kuoverhaul mfumo mzima wa elimu
anamtaka rais aunde commission ya kushughulikia matatizo ya elimu
 
anasema hata ninyi wahadhiri hali yenu ni taabani.
anazungumzia GDP tunayoweka katika elimu, bunge iweke trillioni 3.3 katika bajeti ya elimu. tuweke 10% ya pato la nchi katika elimu
 
tuwekeze kwenye mfumo wa elimu, tuhakikishe usawa katika elimu kama alivyosema prof mkenda. tuwe na elimu inayojenga uzalendo, tanzania tuwe kioo cha afrika. tuheshimu taaluma za watu, pamoja tutashinda.
amemaliza
 
sasa ni rais wa chama cha walimu mkoba.
anauliza elimu yetu inatupeleka wapi?
 
kutumia mtu mwenye elimu dhaifu kufundisha wengine tumeshindwa kabla ya kuanza
 
anakumbushia nadharia ya howard gardner, wa multiple intelligence, hapa tanzania, tunazingatia vipaji mbalimbali?
 
tufanye chochote, sio siku tulirudi kwa Mungu tuonekane tulikuja kuhudhuria tu duniani
 
teja anakaa tu kijiweni halafu anasema eti one day mwanangu nitatoka!
kamaliza
 
zamu ya watu mbalimbali kuchangia. dk. 2, 2
anachangia nchimbi
 
hatutumii tafiti zinazofanyika nchini kwetu (anamnukuu prof. Ishumi)
 
watanzania wengi hatujui kiingereza, si sahihi kukitumia kufundishia
 
rais aagize kiswahili kitumike kufundisha hadi chuo kikuu
 
anachangia frank massawe. anasema elimu ya nchi tumeharibu wenyewe. tulikosea kuharibu elimu ya mwingereza. sio sawa kusoma kwa kiswahili, dunia ya sasa hivi inatumia kiingereza, tanzania sio kisiwa.
kwa nini tuliua darasa la nane? UPE ilikuwa ni useless primary education
turudishe mfumo wa 4 4 2 2
 
anachangia twalipo. sio kila anayetaka kufundisha awe mwalimu. kuwe na board ya walimu
 
anachangia mkulima, anasema kwa kweli hali ni mbaya. baba wataifa hakupenda kusikiasikia, bali alipenda kujua na kuona.
tuache kulalamika bila kwenda field kuona hali halisi
 
Back
Top Bottom