Mjadala wa katiba mpya

Mjadala wa katiba mpya

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Japo mchakato wa katiba haujaanza lakini sio vibaya kuanza kujadili kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa upande wangu ningeambiwa nitaje vitu ambavyo vingewekwa kwenye katiba mpya mimi ningesema hivi:-
1.Mkuu wa jeshi la polisi asiteuliwe na raisi pafanyike usaili
2.Kuwa waziri sio lazima uwe mbunge
3.Mkuu wa mifuko ya jamii asiteuliwe na raisi
4.Spika wa bunge asitokane na vyama vya siasa anaweza hata asiwe na chama na ufanyike usaili
5.Jaji mkuu asiteuliwe na raisi ufanyike usaili
6.Mkuu wa usalama wa taifa asiteuliwa na raisi ufanyike usaili
7.Mkuu wa tume ya uchaguzi asiteuliwe na raisi
8.Sheria ya kusema raisi hawezi shitakiwa kwa makosa ya alipokuwa madarakani iangaliwe upya.Kama ni makosa ya kibinadamu ya kisiasa asishitakiwa mfano mzuri labda siasa ya kuhamisha watu vijijini ilivyoleta madhara huo ni ubinadamu ila makosa makubwa mfano kula rushwa na kufuja mali ya uma aburuzwe fasta

Ni hayo tu hebu na wengine ongeeni nyama.Ila mkuu wa majeshi aendelee kuteuliwa na raisi maana duniani hakuna nchi ambayo raisi sio Amiri jeshi mkuu
 
1. Restructuring ya Muungano - maoni yangu 3 government kama rasimu ya Warioba
2. Ma-judge wasiteuliwe na Rais, watokane na mfumo wa kimahakama ili kuwapata ambapo watafanyiwa usaili

3. Mfumo wa serikali za mitaa ubadilishwe; maoni yangu tuwe na kanda za uongozi ili kumpunguzia mzigo Rais pia kurahisisha maamuzi mfano Mtwara, Lindi, Ruvuma iwe ni kanda moja na Area commissioner atokane na local authorities sio kuteuliwa na Rais. Either achaguliwe na wananchi /apendekezwe na kupitishwa na madiwani

4. Baadhi ya vigezo vya mtu kuwania nafasi ya ubunge vibadilishwe
Mf; kigezo cha kujua kusoma na kuandika, kiongezewe ubora mana mtu akishapita na kuwa mbunge anaenda kuhusika moja kwa moja katika kutunga sheria za nchi yetu pamoja na sera

5. CAG asiwe mteule wa Rais , Apendekezwe na kuteuliwa na bunge, Rais afanye confirmation tu.

6. Hiki kifungu cha kwenye katiba kuwa Rais anaweza kumfutia adhabu mtu yeyote alipatikana na hatia yoyote bila masharti / kwa masharti fulani. Kitazamwe upya
 
Mbona mmeingia mitini nilisahau kipengele kimoja
Raisi aangaliwe historia yake ya nyuma juu ya afya yake kama kuna ka dalili na ugonjwa wa akili
 
Back
Top Bottom