TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini



Kikao cha kuhitimisha mradi wa TUSHIRIKISHANE jimbo la Bukoba Manispaa kilichofanyika tarehe 21/7/2017 kikiwakutanisha Jamii Media, Ofisi ya Mbunge, Halmashauri na wananchi kujadili kwa pamoja hatua zilizofikiwa katika vipaumbele vinne vya TUSHIRIKISHANE ambavyo ni ahadi nne za mbunge, changamoto na mafunzo yaliyotokana na mradi huu katika jimbo la Bkoba Mjini.

Ripoti kamili itawekwa hapa baada ya kukamilika.
 
??????????. Cha kuhitimisha? Ngoja tuone tunahitimu cheti chetu kikiwa na A,B,C,D ama F
 
Jamii Media imeendesha semina ya Uendeshaji na Usimamizi wa Mijadala Huru (Meza ya Duara) katika Manispaa ya Bukoba leo tarehe 25/7/2017 ikiwa ni sehemu ya mradi wa Tushirikishane. Washiriki wa semina ni wajumbe wa vijiwe mbali mbali katika manispaa ya Bukoba na muwasilishaji alikua ni ndugu Wistone Mogha kutoka Kigoma - Ujiji ambao ndio waanzilishi wa Meza ya Duara. Mwitikio ulikua ni mzuri tunategemea kuanzishwa kwa Meza ya Duara ambayo itakua chachu ya mijadala huru katika manispaa ya Bukoba

 
Leo tarehe 26.07.2017 mbunge alikuwa na mkutano maeneo ya soko kuu mbona hatupati mrejesho

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu, mimi ni Afisa Mawasiliano wa Jamii Media sio wa Mbunge. Taarifa ya mkutano ataleta hapa Mbunge au Katibu wa Mbunge. Hili ni jukwaa la wanaBukoba wote na sehemu sahihi kwa ofisi ya Mbunge, Halmashauri na taasisi nyingine kuwasilisha taarifa zao kwa wananchi. Aidha, nimepata picha chache za mkutano huo;
 
Mkuu hii ni Tanzania yetu sote bukoba ni sehemu ya Tanzania hivyo tumeanzisha mjadala huu kuikumbusha serikali wajibu wake.Na wewe haukatazwi kuanzisha Wa kwako hakuna sehemu ya tz ambayo haina matatizo nadhani umenielewa
Ww kama mzaliwa wa uko umechukua hatua gani, kuleta matokeo chanya?! Ivi hadi usafi tu mnasubili serikali?! Poor wahaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ww kama mzaliwa wa uko umechukua hatua gani, kuleta matokeo chanya?! Ivi hadi usafi tu mnasubili serikali?! Poor wahaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wahaya for what mdau? Kama huwataki si unaachane nao kiroho safi tu ama wamekufata wakaja kukuomba msaada?

Shughurikia ya kwako na waachie hao unaowaita "wahaya" wafe na ya kwao. Jali sana mda wako binafsi kuliko ya hao unaowaita "wahaya".
 
Hivi waislam wa Bukoba mjini kama Alhaji Kichwabuta na wengine wako wapi? Au mnawatenga? Washirikishe
 
Abantu ba Bukoba, mwagira mayo.........
Any updates???
 
Hivi stendi na soko vimefikia wapi?
 
Unafiki wa wanakagera na bukoba ni kwamba hawajui ni nan hasa anaweza kuwakwamua,

Lwakatare huyu huyu aliyeshindwa na kula hela ya michango ya abana bashome ndo mnategemea mazuri kwake?

Ngoja tusubiri ntarudi hapa miradi ikianza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…