MWENDELEZO WA UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA 4. Kama tulivyoona awali mradi wa maji kigoma ujiji ulikuwa umesimama toka mwezi machi mwaka 2015 ambapo ndio ulipaswa kumalizika. Lakini kwa jitahada za mbunge tukaona mradi huo umeanza kutekelezwa. Mradi huu ulikuwa katika ahadi za mbunge na sasa umefikia hatua za mwisho na tulitegemea ungemalizika mwezi Disemba 2016 lakini mradi huo umeanza tena kusuasua.
BUNGENI LEO KAMA SWALI NAMBA.(46) Mheshimiwa Zitto Ruyagwa Kabwe ameuliza;-
Mradi wamaji wa manispaa ya kigoma unaogharimu zaidi shillingi billion 32 ambao unafadhiliwa na shirika la KFW la ujerumani na jumuiya ya ulaya ulipangwa kukamilika mwezi Machi 2015:
(a)Je, kwanini mradi huu umechelewa kukamilika kwa mujibu wa mkataba;
(b)Je, Serikali inachukua hatua gani dhidi ya mkandarasi kwa kuchelewa kukamilisha mradi huo.
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Akajibu
Mheshimiwa Spika,naomba kujibu swali la mheshimiwa zitto Ruyagwa kabwe lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-
MHESHIMIWA SPIKA, Mradi wa maji wa manispaa ya kigoma unagharimiwa na serikali kwa kushirikiana na umoja wa ulaya na serikali ya ujerumani kupitia benki ya maendeleo ya KFW kwa gharama ya Euro million 16.32 sawa na shillingi billion 39.13
MHESHIMIWA SPIKA, Ujenzi wa mradi huu unaotekelezwa na mkandarasi SPENCON SERVICES LTD ulianza mwezi machi 2013 na ulitarajiwa kukamilika mwezi machi 2015. Hata hivyo baada tu ya kuanza kwa ujenzi , mkandarasi alichelewa kupewa eneo la ujenzi kutokana na matatizo ya fidia. Hali hii ilisababisha mkandarasi kupewa nyongeza ya muda wa kazi hadi kufikia nwezi December,2015. Pia kubadilika kwa menejiment ya SPENCON SERVICES LTD na mtaji mdogo kifedha kumechangia kuchelewa kwa ukamilishaji wa mradi wa maji ambapo hadi kufikia mwezi Oktoba 2016 utekelezaji wa mradi ulikuwa umefikia wastani wa asilimia kubwa.
MHESHIMIWA SPIKA, Kwa kuzingatia masharti ya mkataba, Serikali imechukua hatua dhidi ya mkandarasi ikiwa ni pamoja na kumkata fidia (liquidated damages) ya Euro 1,632,315.27 sawa na billion 3.9 ambayo ni asilimia 10 ya mkataba kuanzia mwezi januari 2016. Vilevile mkandarasi ameagizwa kuongeza nguvu kazi, vifaa na pia kufanya kazi muda wa ziada zikiwemo siku za mapumziko pia mkandarasi ameandikiwa barua ya kumfahamisha kuwa Wizara imemuweka katika kundi la Non Performing Contractors na mamlaka zinazohusika za PPRA na CRB zimejulishwa.
MHESHIMIWA SPIKA, Kwa kuwa miundombinu ya msingi kama manteki amekwisha jenga,pampu zote ameleta, wananchi wa kigoma mjini wataanza kupata maji kuanzia mwezi April,2017.
KATIKA SWALI KA NYONGEZA
Zitto Kabwe ameuliza kuhusu kuweka solar pumps za kusukuma maji ili kupunguza gharama za uendeshaji na pia ameomba kuunganisha mji mdogo wa Mwandiga katika mradi huu wa maji wa manispaa ya kigoma ujiji. Tunashukuru kuutarifu Umma kuwa serikali imekubali kuwa itachukua ushauri wa mbunge wa kutumia umeme wa jua katika kusukuma maji ili kupunguza gharama na pia serikali imekubali kuunganisha mji wa Mwandiga kwenye mradi huu wa maji wa manispaa ya kigoma ujiji