TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigoma Mjini

Kigoma mko vizuri, naona mipango kazi yenu itaifanya Kigoma kuwa kama Dubai huko mbeleni.
 
Thread za maendeleo hazichangamkiwi kama zile za matukio hasa matukio hasi....Binafsi nimesoma kuanzia mwanzo na nimefurahi sana. Msichoke kutupa mrejesho wa yaendeleyayo. Zitto akiwekaga siasa cheap pembeni, yuko njema sana. Wananchi nawashauri kupokra haya positively na wajitoe zaidi maana Kigoma itajengwa na wakazi wake. Asante
 
Kigoma mko vizuri, naona mipango kazi yenu itaifanya Kigoma kuwa kama Dubai huko mbeleni.
Karibu sana kigoma. Fursa za kuwekeza na biashara mbalimbali na nchi jirani kama congo na burundi zinabadilisha kabisa kipato cha watu kwasasa. Karibuni kigoma
 
Jukumu letu ni kuwaunga mkono kwenye mchakato huu wa maendeleo
 
Kigoma inapaswa kuwa jiji kuu ukanda wa magharibi ya Tanzania:
1.Nchi za DRC,Burundi na Rwanda wanaweza kuwa wanakuja na kupitia Kigoma kabla ya kwenda miji mingine ya Tanzania.
2.Nchi nilizozitaja hapo juu zinaweza kuwa wateja wa bidhaa za kilimo na viwanda,endapo Kigoma itatenga maeneo ya viwanda.
3.Kigoma inastahili kupewa uwanja wa ndege za kimataifa ili kuhudumia nchi jirani.
Tatizo la Kigoma,kila mwananchi ni mjuaji na ubishi,hali inayochangia migogoro ya ardhi isoyoisha.
Utatuzi wa ardhi:
Mji wote wa Kigoma na maeneo ya nje ya mji yapimwe kwa sattelite
 
Kesho baraza la ardhi la Manispaa linazinduliwa
 
Waziri wa ardhi akisalimiana na mbunge wa kigoma mjini Zitto Kabwe baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kigoma leo.
 
Video za mbunge akijibu maswali tayari zimepandishwa rejea kwenye maswali hapo juu kuona majibu ya Zitto Kabwe moja moja. Karibuni
 


Waziri wa ardhi nyumba na makazi Ndg Wiliam Lukuvi akizindua jengo la Baraza la ardhi la wilaya ya kigoma akiwa na mbunge Zitto Kabwe
 
Hii imekaa vizuri ila nina wasiwasi na uchu na tamaa ya Meya wetu. Tukimdhibiti Meya tutafika, tukimuacha ashirikiane na wala rushwa basi manispaa yetu itaongoza kwa rushwa!
 
Nikiwa kama M/Kiti wa Mipango Miji nikitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya migogoro ya Ardhi iliyowasilishwa kwa Waziri wa Ardhi Mh. Lukuvi.

Katika kushughulikia migogoro ya ardh, nimejifunza kuwa wananchi wanawasilisha matatizo yao ya Ardhi nasi tunayatafutia ufumbuzi/Usuluhishi lakin anapokuja kiongozi mwingine wao huwasilisha matatizo yalokwishapatiwa majibu kwa viongozi hao.

Nimeona migogoro tuloishughulikia kama Manispaa na ilishughulikiwa na Mkuu wa wilaya aliyeobdoka na ikapatiwa ufumvuzi. Lakini alipokuja DC na RC mpya wananchi waliipeleka tena na ikapatiwa ufumbuzi kisha watu hao hao tena wameiwasilisha kwa Waziri.

WITO WANGU
Nawaomba wananchi wajenge imani kwa viongozi wao walotupa dhamana ya kuwatumikia. Tumejipanga vizuri kuhakikisha haki ya kila mtu inapatikana.

Kupitia kamati yangu ya Mipango miji tunapokea migogogoro ya Ardhi na kuipatia masuluhisho na tutahakikisha wenye stahiki zao wanazipata.

Kwa wale tulomaliza maswala yao ya fidia nawaomba muwe wavumilivu kwani kwa sasa Halmashauri ya Manispaa haina Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kulipa fidia. Mwaka ujao wa Fedha tumekusudia kutenga bajeti kulipa fidia kwa wananchi tulosikiliza migogoro yao na kuona wanastahili kulipwa fidia baada ya Ardhi yao kutwaliwa na serikali kwa matumizi mbalimbali.

Tunajali utu na haki za watu na tutazilinda

Butije H. Butije
M/Kiti wa Mipangomiji
Manispaa ya Kigoma Ujiji
 
Reactions: B2j
Katika kuhakikisha tunamaliza migogoro ya Ardhi hapa mjini, tumeshauriana na Mkuu wa wilaya tushirikiane kwa pamoja ili migogoro inayowezekana kutatuliwa ktk ngazi ya Halmashauri tuitatue kwa haraka ili wananchi wetu wapate haki zao na waendelee na shughuli za uendelezaji wa Ardhi zao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
 
kwanza niwapongeze kwa kazi nzuri, lkn nataka nijue ni kigezo gani mnachotumia kujenga barabara za lami mwanga, gungu, kigoma na ujiji kujenga za mawe!!!!!! pili ni fikra gani bunifu iliyowafanya mjenge mfeteji wa maji ghali kwa concrete kuanzia mwanga kwa mchaga hadi kwa bidiyanguze!!!!!!!
 
M/Kiti wa Mipango Miji Butije H. na Diwan viti Maalum Ndugu Tatu R. Amani wakisishiriki zoezi la urekebishaji wa barabara ya Mtaa wa wauza mitumba Mwanga Sokoni.

Ubovu wa Barbara hiyo umekuwa ni kero kubwa sana kwa wafanyabiashara wa Soko la Mwanga.

Baada ya kurekebisha njia hiyo vema tutapeleka vifusi vingine kusawazisha Barabara hiyo ikae vema.

Butije Hamis
 
Huu ndio mfano wa kuigwa kwa viongozi wetu, wanapaswa kushirikiana na viongozi wengine kuleta maendeleo na kutimiza ahadi zao walizotoa pia kutoa feedback na kuwa na forum kwa ajili ya kujibu maswali ya wananchi wao.Kudos to Jamii Forum,Mh Zitto, Meya wa kigoma na viongozi wengine.Hii inatia moyo kwa kweli
 
Ziara Yangu Mkoani Arusha Leo

Leo mchana nilikuwa mkoani Arusha Kwaajili ya kutekeleza majukumu na kazi zangu kama Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini (Ujiji). Ziara yangu mkoani Arusha ilikuwa makhsus kwaajili ya kutembelea Chuo cha Kilimanjaro International Information Technology & Computing College (KIITEC).

Jimboni Ujiji tuna lengo la kuwa na chuo cha Ufundi cha namna hii, kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwaongezea maarifa vijana wetu kupitia kozi mbalimbali zinazotolewa na vyuo vya aina hii. Nawashukuru sana KIITEC, nimejifunza, Ujiji tutajitahidi kuiga jambo hili zuri la watu wa Arusha.


Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Arusha
Disemba 2, 2016
 
KATIKA UTEKELEZAJI WA AHADI NYONGEZA NAMBA MBILI Waziri wa Nyumba na maendeleo Mhe.William Lukuvi ametoa kauli ya juu ya wakazi wanaoishi Eneo la sanganyigwa Mlima kibirizi kata ya kigoma mjini ktk mkutano wa wananchi mwanga centre kuwa itakuja Timu ya wataalamu kutoka Wizarani idara mbalimbali wa Mipango miji,Ardhi na udhamini na Mazingira kuja kufanya utafiti na kujua kinachojaza mchanga Ziwa Tanganyika kama ni wakazi watapisha eneo la Mlimani na kulipwa fidia inayostahiki sheria inavyosema kama Hawajazi ziwa watabaki eneo hilo kwa Maisha yao na vizazi vyao. pichani ni waziri akiwa sambamba na Diwani wa kata hio Ndg Hussein Kalyango
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…