TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigoma Mjini

Madiwani wa manspaa ya ujiji/kigoma wa kamati ya fedha na uongozi wametembelea ujenzi wa madarasa 5 mapya na Madawati 100 na Matundu ya choo 12 na Ukarabati wa madarasa ya shule ya msingi KABINGO KATA YA GUNGU ujenzi uliogharimu Shs milion125 hali ya mradi nizuri tunategemea wanafunzi kuingia mapema sana,
Mstahiki meya na madiwani na wataalamu wamewambia kamati ya shule kufanya haraka ujenzi ukamilike wanafunzi wasome kwani darasani wamejaa wanafunzi wengi ili wanafunzi wasome kwa nafasi na miongozo ya Elimu.
Meya amewambia walimu manspaa imeanzisha mashindano ya kinyago cheusi kwa shule za mwisho yani tatu ya mwisho nikinyago na wanaongoza watapewa zawadi ya fedha na kawaomba walimu kufundisha kwa bidii.
 
Madiwani wa manspaa ya ujiji/kigoma wajumbe wa kamati ya fedha na uongozi wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa mfereji wa Maji ya mvua KATUBUKA kata ya MWANGA KASKAZINI uliogharimu Milioni 771,840,000 ujenzi wake unaendelea na mradi unasimamiwa na manspaa ya ujiji/kigoma ulionusuru Nyumba takiliba kumi na tano zilizokuwa zinapitiwa na maji na sasa zimesalimika kuanguka.
mstahiki meya amewaambia wakazi wanaopitiwa na mfereji kuwa walinzi wa miundombinu kwa mtu atakae haribu mradi huo kwa lengo la hujuma yoyote,Manispaa imetatua malalamiko yao ya muda mrefu yaliyokua yanatishia nyumba zao na mali zao,Eneo hili lilikua hatari sasa ni salama barabara inapitika vizuri. Ahadi ya mhe Mbunge zitto kabwe na Diwani baba levo imetekelezwa
 
Madiwani wa manspaa ya ujiji/kigoma wajumbe wa kamati ya fedha na uongozi wakiongozwa na mstahiki meya wametembelea mradi wa ujenzi wa MADUKA YA TIKETI NA UKUTA UTAKAOZUNGUKA KITUO CHA MABASI MASANGA kata ya GUNGU Kwa Gharama ya milion 849,690,000 mradi upo unaendelea na lengo la manspaa nikuongeza mapato na kutoa huduma kwa Abiria wanaosafiri nje ya mkoa kupata huduma nzuri na salama.
mradi wa maduka 32 yatakapo isha utatolewa utaratibu wa kuyapangisha kwa makampuni ya mabasi na mawakala wa tiketi manspaa ya ujiji/kigoma.
 
Madiwani wa manspaa ya ujiji/kigoma wajumbe wa kamati ya fedha na uongozi wametembelea Eneo lliloteuliwa kujenga HOSPITALI YA WILAYA ktk manspaa.
Eneo hili ndio ujenzi utajengwa wodi na hopitali ktk kata ya RUSIMBI Maandalizi ya kujipanga na kuwa na hospitali kama Ahadi ya mhe.mbunge na Diwani kwa wanachi wa kigoma mjini. jina HOSPITALI YA WILAYA RUSIMBI
 
Madiwani wa manspaa ya ujiji/kigoma wajumbe wa kamati ya fedha wametembelea na kukagua uzalishaji wa Barafu MWALO WA KIBIRIZI kata ya KIBIRIZI Nakuangalia namna mradi huu utawasaidia wavuvi kuifadhi samaki bila kuaribika watakapo kwenda kuvua samaki au kusafirisha kwenda mikoani.
mstahiki meya na Diwani wa kata ya kibirizi wamefurahi kukamilika kwa mradi huu utawasaidia wavuvi na kupandisha dhamani ya mazao ya uvuvi ktk manspaa ya ujiji/kigoma amewakikishia wavuvi watashughulikia kero za wavuvi na kuwaomba watumie mwalo wa kibirizi utanufaisha sana.
kero ya kutekwa na kunyanganywa vifaa vya uvuvi wameomba vyombo vya usalama kuwalinda wavuvi wetu kwani ziwa ndio kiwanda chetu kigoma.
 
Madiwani wa manspaa ya ujiji/kigoma wajumbe wa kamati ya fedha na uongozi wametembelea na kukagua ujenzi wa BARABARA YA RUSIMBI kata ya RUSIMBI km 1 kwa kiwango cha LAMI Kwa Gharama ya Tshs Bilion 2,567,376,000 mradi huu utapitia soko la kwanoti,Msikiti meli mpaka OFISI YA ACT WAZALENDO MKOA kutakuwa na mkutanio ya barabra ya lumumba na Mahakama ya ujiji.
mstahiki meya na Diwani wa Rusimbi wamemtaka mkandarasi kuongeza nguvu kwani kasi ni ndogo wananchi wanataka kuona na kupita kwenye barabara ya lami iliwaijenge kigoma na ujiji.wataalamu wa manspaa wamewatoa hofu wakazi wa ujiji na kuwaambia mkandarasi anaongeza vifaaa.ujenzi utakamilika kwa wakati
 
Madiwani wa maspaa ya ujiji/kigoma wajumbe wa kamati ya fedha na uongozi wamefika kuangalia ujenzi wa korongo wa LUBENGERA kata ya KIGOMA maandalizi ya vifaa vya ujenzi wa mfereji wa lubengera mpka stesheni unajengwa kuanzia makao makuu ya ccm mkoa mpka ziwani kwa Gharama Milion 580,020,000 ni Ahadi ya mhe. Diwani Hussein kalyango inaanza kutekelezwa na kunusuru nyumba za wakazi wa lumumba na soko la kigoma.
mhe.diwani aliwakumbusha wataalamu kuangalia ubora wa ujenzi kwani maji yanayopita lubengera ni mengi nayana history kubwa. Ujenzi wa ubabaishaji hautakiwaki kwani wanapaswa kuheshimu taaluma zao na misingi ya utumishi. wanachi wa kata ya kigoma wawe watulivu mkandarasi ameanzaa ujenzi na kero inakwisha.
 
Ujenzi wa Barabara ya RUSIMBI Inayopita kata 6 za Manspaa ya ujiji/kigoma ambazo ni RUSIMBI,MAJENGO,KASINGIRIMA,MACHINJIONI,RUBUNGA, NA KASIMBU Km 1 kiwango cha lami ujenzi umeanza leo tarehe 01/02/2017 barabara hiyo inapita Kwa noti,Msikiti meli mpka Ofisi ya Act wazalendo mkoa wa kigoma.
Mkandarasi ameanza ujenzi wa barabara ya lami njia za watembea kwa miguu na Taa za barabrani.
 
Nimafanikio makubwa kwa mkoa wa kigoma kushika nafasi 4 kati ya 10 bora matokeo ya kidato cha NNE 2016, Hongera kwa wahusika wote hasa walimu wetu kwa kazi kubwa na iliyotukuka mliyoionyesha.
Hongera manispaa ya kigoma Ujiji ingawa si yakujivunia kwa kiasi kikubwa bali kutoka nafasi ya 82 kati 168 kwa 2015 hatimae nafasi ya 31 kati ya 178 kwa 2016 kitaifa, nijambo linalotia faraja ya mafanikio ndani ya siku zijazo kushika nafasi ya juu zaidi kulingana na mikakati na malengo makubwa tuliyojiwekea ndani ya Halmashauri.
Kwaniaba ya wazazi niendelee kuwapongeza walimu na wadau wote kwa kazi kubwa mnayoifanya kwa manufaa ya vizazi vyetu vya leo na kesho.

Ahsante
Hussein Ruhava
Mayor Kigoma Ujiji.
 
Mstahiki Meya Hussein juma Ruhava wa Manispaa ya ujiji/kigoma na Wajumbe wa kamati ya fedha na Uongozi Afisa Elimu sekondari, Afisa Elimu msingi,Waratibu Elimu kata,Walimu wakuu shule za msingi, Wakuu wa shule za sekondari na Maafisa Mbali mbali Idara ya Elimu.
Wakizungumza na Wajumbe wa kamati ya fedha juu ya kuongeza ufaulu na kupongezwa kwa kufaulisha vizuri mwaka 2017 kusikiliza kero mbali mbali pamoja na kutoa ufafanuzi wa malipo ya Fedha za Uhamisho kwa waalimu.
Mstahiki meya Amewapongeza walimu wote wa shule za sekondari na Msingi kwa kujitolea kuwafundisha wanafunzi kwa moyo safi na kuwaomba kuvumilia kwani serikali inafanyia kazi Madai yao.
Ufaulu kwa shule za sekondari za manispaa ya ujiji/kigoma tumetoka 31 kati Halmashauri 178 Mwaka 2017 kwa inchi nzima.Kimkoa tumekua wa 4.
Tunawaomba kuendelea kujitolea kufundisha tunajua mnachangamoto nyingi na tutazitatua mpaka zitakwisha tushirikianeni kwani watoto ni wetu
 
Tutakuwa na mkutano wa Meza ya Duara huko Kigoma leo Jumanne kuanzia saa 11 jioni. Mkutano huu ni sehemu ya Offline Strategy ya mradi wa Tushirikishane.


Washiriki ni wana Kigoma Mjini na mgeni wa mjadala atakuwa Winston Mogha, Afisa Mawasiliano wa Tushirikishane mjini humo. Tunakamilisha mawasiliano ili MD naye aweze kushiriki mubashara kwenye mjadala kutokea Dar.
Updates zitatolewa kupitia mnakasha wa Jimbo la Kigoma mjini uliopo JamiiForums.com

TUSHIRIKISHANE - Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigoma Mjini

Asante.
 
Mwaliko wa Kushiriki Mjadala wa Maendeleo ya Mradi wa Tushirikishane Jimbo la Kigoma kupitia Meza ya Duara—Tanganyika


Tutakuwa na mkutano wa Meza ya Duara Jimbo la Kigoma leo Jumanne kuanzia saa 11 jioni. Mkutano huu ni sehemu ya mkakati wa Mradi wa Tushirikishane katika kuwafikia wananchi wasiokuwa na mawasiliano ya mtandao.


Wana Kigoma Mjini na wote wenye maslahi na maendeleo ya Jimbo hili wanaalikwa kushiriki moja kwa moja au kwa njia zitakazotolewa hapa chini. Mgeni wa Mjadala wa leo atakuwa Ndg. Winston Mogha, Afisa Mawasiliano wa Tushirikishane Kigoma Mjini. Pia ndg. Maxence Melo, Mkurugenzi wa Jamii Media, atashiriki mubashara kwenye mjadala kutokea Dar.


Kwa wale ambao hawataweza kufika kwenye eneo la mjadala, wanaweza kufuatilia yatakayojiri kupitia mitandao ifuatayo:


Jamiiforums.com link TUSHIRIKISHANE - Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigoma Mjini

Facebook link Tushirikishane | Facebook ID Tushirikishane

Twitter link Tushirikishane (@tushirikishane) | Twitter IDTushirikishane


Nyote mnakaribishwa!
 
Tunajenga Manispaa kwa misingi ya Ujamaa

[Sehemu ya Hotuba Yangu kwa Wananchi Wenzangu wa Kata ya Kagera]

Wananchi wa Kata ya Kagera, Leo pamoja na mambo mengine nitazungumza nanyi kuhusu Mradi mkubwa wa Umwagiliaji kwenye Delta ya Mto Luiche. Mradi huu upo kwenye kata yenu. Wakati wa kampeni niliwaahidi kwamba tutajitahidi kuendeleza Bonde la Mto Luiche ili kuzalisha chakula cha kutosha kwa kulisha mkoa wetu wa Kigoma, mikoa mengine nchini pamoja na nchi jirani.

Mwaka jana nilifanikiwa kupata mawasiliano kutoka Nchi ya Falme ya Kuwait kwa nchi yetu kupitia Wizara ya Mambo ya nje. Serikali ya Kuwait ilitoa dhamira yake ya kutoa fedha kuendeleza Delta ya Mto Luiche ili kuzalisha Mpunga, Mahindi na mbogamboga. Baadaye niliwasiliana na Wizara ya Kilimo na kisha Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Pia nilizungumza suala hili Bungeni mara mbili katika kuweka msisitizo wa umuhimu wa mradi huu.

Mradi huu utagharimu Fedha za kigeni USD 15 milioni sawa sawa na shilingi 31 bilioni. Fedha zote hizo Mfuko wa Wakfu wa Kuwait (Kuwait Fund) utagharamia baada ya Serikali ya Tanzania kulipia gharama za kuandaa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina (detailed design). Mwaka 2016/17 ndio nilipambana bungeni na kushirikiana na watendaji wa Kamisheni ya Umwagiliaji na Waziri wa Umwagiliaji kupata fedha hizo (za kufanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi).

Bahati mbaya sana mpaka mwezi Disemba mwaka 2016, Tume ya Umwagiliaji ilikuwa imepata 13% tu ya fedha za maendeleo kutokana na Hazina kuchelewa kutuma Fedha za Maendeleo kwenye Wizara, Idara na Wakala wa Serikali. Bahati nzuri katika uchache huo wa Fedha Tume imeanza kazi ya kutimiza masharti yaliyotolewa na Serikali ya Kuwait ili kuendeleza mradi huu wa Mpunga katika Delta ya Mto Luiche. Hivyo mradi huu unaendelea na tutaupigania ukamilike.

Tutatekeleza mradi huu kwa misingi ya Ujamaa

Mradi wa Umwagiliaji wa Delta ya Mto Luiche utakuwa na ukubwa wa Hekta 2800 za Mpunga, 150 za Mahindi na 50 za mboga mboga (horticulture). Utekelezaji wa Mradi huu utafanywa kwa misingi ya itikadi na sera za kijamaa ambapo tutafanya kilimo cha Ushirika (integrated production system). Jumla ya familia 1400 zitagawiwa hekta 2800 za kulima mpunga ambapo kila familia itapata hekta 2 ambazo zimeshawekewa miundombinu yote muhimu ikiwemo mifereji ya maji na miundombinu ya umwagiliaji. Wakulima wataunda Ushirika na kupitia Ushirika wao watajiunga na Skimu ya Hifadhi ya Jamii ili kuweza kupata mikopo ya pembejeo, Bima ya Afya na kuweka akiba ya uzeeni.

Hakuna mwananchi aliyeko kwenye Bonde la Luiche hivi sasa ataondolewa katika utekelezaji wa mradi huu. Lengo ni kuwapa uwezo watu masikini kuondokana na umasikini wa sasa na wa baadaye kwa kupitia mfumo madhubuti wa Hifadhi ya Jamii.

Mabepari wangegawa Bonde zima kwa tajiri mmoja na kugeuza wananchi wetu vibarua wa shamba la tajiri. Sisi ACT Wazalendo tunawawezesha wananchi kuzalisha mali na kuendeleza maisha yao. Licha ya kutoa kipaumbele kwa wananchi wenye ardhi ndani ya Delta, mgawo wa mashamba hayo ya hekta 2 kila familia utafanywa kwa uwazi mkubwa na watu masikini watapewa kipaumbele.

Mradi wa Mpunga katika Delta ya Mto Luiche utazalisha kwa mwaka Mara 2 jumla ya tani 32,000 za mpunga kwa mwaka na hivyo kuingiza pato ghafi la takribani shilingi 16 bilioni kwa mwaka kwa wakulima kwenye ushirika wao. Huu ni wastani wa pato la shilingi 11 milioni Kwa mwaka Kwa kila familia na hivyo kuwezesha familia nyingi kuondoka kwenye umasikini na kuwa na kipato cha kati. Kupitia hifadhi ya jamii ushirika unaweza kumiliki kinu cha kukobolea mpunga na kuongeza mapato zaidi Kwa wanachama wake.

Nawataka wananchi wa Kata ya Kagera kujiandaa kuupokea mradi huu ili tuweze kujikomboa. Mradi huu utakuwa na bwawa litakalotumika kuzalisha umeme na barabara za kuelekea na kuvuka mto Luiche zitajengwa katika ujenzi wa mradi. Haya Ndio maendeleo tunayotaka Kwa wananchi wetu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ili tusonge mbele.

Naamini diwani wenu pia amewaeleza kuhusu utekelezaji wa mfumo wa Hifadhi ya Jamii wa Manispaa yetu ambapo tunatumia Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo na 10% ya mapato ya manispaa Kwa Vijana na Wanawake kulipia nusu ya michango yenu kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii. Mfuko wa NSSF na Mfuko wa PSPF tayari wameanza kuandikisha vikundi vya vijana na wanawake katika Skimu yetu hii.

Wanachama watafaidika na Bima ya Afya na Mikopo nafuu kuendeleza shughuli zao za uzalishaji kupitia vikundi vyao. Nawaomba tushirikiane kujenga manispaa ambayo kila mwananchi wake ana Bima ya Afya. Inawezekana, kila mtu atimize wajibu wake.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Ziarani Kata ya Kagera
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Machi 11, 2017
 
Ujenzi wa madarasa Shule ya msingi Bangwe umeanza leo, tumeanza kwa kujenga msingi wenye madarasa mawili baada ya kupokea fedha jumla ya 11,300000 kwaajili ya Darasa moja na kuunganisha nguvu za wadau na wananchi wa kata ya Bangwe kuchangia ujenzi wa msingi wa Darasa moja nimatumaini yangu kwamba juhudi zilizofanyika kuchangia ujenzi wa msingi Darasa moja zitaendelea katika kuchangia kupandisha na ukamilisha wa Darasa hilo hatimae kuwa na madarasa mawili yatakayokidhi lengo la hitajio kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kuwa na madarasa 2 katika shule hii.
Hussein J. Ruhava
Diwani wa Kata ya Bangwe
Meya kigoma ujiji.
 
 
Katika utekelezaji wa ahadi ya mbunge ya kuwezesha kina mama na wajasiriamali katika kuhakikisha vikundi vyao vimesajiliwa na vinaweza kukopesheka. Mbunge akishirikiana na madiwani waliweza kutembelea vikundi mbali mbali pamoja na maafisa wa mfuko wa Hifadhi ya jamii wa NSSF ili kuwawezesha kina mama kupata bima za afya na kuwaelekeza namna ya kujisajili ili waweze kukopesheka. Katika utaratibu wa kupata bima za afya toka Nssf mbunge atachangia asilimia 40 na asilimia 60 toka kwenye halmashauri. Pichani ni picha zikionyesha kata mbili ya kigoma mjini ya Bwana Hussein Kalyango wa kata ya kigoma mjini na Ruhomvya Yunus wa kata ya kibirizi.
 
Bonyeza link hio ya blue ili uweze kushiriki moja kwa moja na mbunge wako Ndg zitto kabwe. Atajibu maswali yote yahusiyo maendeleo jimboni kwake changamoto na mafanikio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…