Mjadala wa Ubatizo unatoka wapi kwenye Biblia?

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
276
Reaction score
460
Mimi sio msomaji mzuri wa Biblia lakini nikipata muda kidogo huwa natulia kusoma baadhi ya vitabu vya Biblia.
Leo nimesoma kitabu cha Matendo ya mitume kinachozungumzia maisha na matendo ya wafuasi, wanafunzi na mitume wa Yesu baada ya kifo chake.

Kitabu hiki kinaonyesha namna wayahudi na makabila ya karibu walivyoipokea injiri baada ya kifo cha Yesu na kufufuka kwake.

Nilipata jambo la kujiuliza niliposoma sura ya 9 aya ya 17-19 kitabu cha Matendo ya mitume inavyoeleza ubatizo wa Sauli wa Tarso alivyofika Dameski.

Inaeleza kuwa Anania alimbatiza Sauli nyumbani na Sauli akapata kuona na akajazwa nguvu za roho Mtakatifu, akala akala chakula na kupata nguvu.

Narejea kwenye kitabu kwa kunukuu "Anania akaenda zake akaingia mle nyumbani akamwekea mikono akisema, ndugu sauli Bwana amenituma, Yesu yeye aliyekutokea kwenye njia uliyoijia, upate kuona tena, ujazwe Roho Mtakatifu, mara vikaanguka machoni pake vitu vitatu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa akala chakula na kupata nguvu" mwisho wa Kunukuu.
Kwa mujibu wa kifungu hiki anania alibatizwa nyumbani, hakuna kielelezo chochote kinachooneshwa kuwa alitolewa mahali pale kupelekwa mtoni au sehemu yenye maji mengi, labda kama nyumba Ile ilikuwa na kisima ndani, pia kifungu hiki hakielezi Sauli alibatizwa kwa maji au kwa ishara gani.

Kifungu hiki kikanikumbusha mabishano yaliyopo baina ya waamini kuwa ubatizo uliothibitishwa kwenye Biblia ni wa maji mengi pekee ambao Yesu kristo alibatizwa.

Nimekumbuka pia maneno ya Yohana mbatizaji wakati wa ubatizo wa yesu aliposema "kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba, bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi.., atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto" Mt 3:11-12.

Vifungu hivi viwili vya ubatizo wa Sauli na Yesu pamoja na maneno ya
Yohana mbatizaji vinanipa mjadala.
Mosi, kuwa ubatizo ni ishara tu ya kuingia kwenye Imani, kwamba inawezekana watu wasibatizwe kwa maji bali Roho Mtakatifu na moto kama alivyosema Yohana?
Pili kwamba maji yanaweza yasitumike kama ishara ya ubatizo na wakati ujao akija yule Mkuu kuliko Yohana?

Je mjadala wa ubatizo wa maji mengi na machache una uhalali gani mbele ya Biblia kwa kuhiasianisha ubatizo wa Sauli na ule uliofanywa na Yohana?

© Peter Mwaihola
IMG_20250119_183926_706~2.jpg
Hoj
 
© Peter MwaiholaView attachment 3207115Hoj
Vifungu hivi viwili vya ubatizo wa Sauli na Yesu pamoja na maneno ya
Yohana mbatizaji vinanipa mjadala.
Mosi, kuwa ubatizo ni ishara tu ya kuingia kwenye Imani, kwamba inawezekana watu wasibatizwe kwa maji bali Roho Mtakatifu na moto kama alivyosema Yohana?
Pili kwamba maji yanaweza yasitumike kama ishara ya ubatizo na wakati ujao akija yule Mkuu kuliko Yohana?

Upo sahihi sana kwa maelezo yako hapo juu na ndivyo ilivyo: Ubatizo siku hizi zetu za Agano Jipya ni Ubatizo wa Roho na Moto au Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Ubatizo wa Maji ni ule wa Agano la Kale, Ubatizo wa Yohana. Kwa hivyo maji mengi au machache sio hoja tena.
 
Back
Top Bottom