Mjadala: Wajasiriamali na Mpango wa Akiba ya Uzeeni na Mafao Mengineyo

SongambeleEN

Member
Joined
Mar 23, 2013
Posts
25
Reaction score
12
Wanabodi,
Kwa kuwa wengi wetu tulidhubutu/tumedhubutu kuitathmini dhana hii ya ujasiriamali sambamba na kujitathmini binafsi juu ya njia sahihi zaidi za kufikia mafanikio ya kweli maishani. Tathmini ambayo ilitupelekea/imetupelekea, kudhubutu kufanya maamuzi sahihi ya kujiajiri wenyewe iwe ni katika mfumo ulio rasmi na ule usio rasmi.

Na kwa kuwa mikiki mikiki ya shughuli hizi za kujiajiri wenyewe zinategemea sana afya bora, nguvu, akili na ustahimilivu wa hali ya juu, sifa ambazo mwanadamu anaweza kupungukiwa kwa kadri siku zinavyokwenda mbele, au kadri anavyozeeka. Sasa basi kwa kuzingatia kuwa wajasiriamali wengi waliojiajiri wenyewe hawajajiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii, njia ambayo ingewawezesha kupata mafao pindi wanapozeeka au kupoteza uwezo wa kuzalisha.

Na kwa kuzingatia kuwa suala la uzee au kupoteza uwezo wa kufanya shughuli za uzalishaji ni mojawapo ya vitu ambavyo sisi kama wajasiriamali hatuna mamlaka navyo, (yaan kuamua visitokee au vinginevyo) isipokuwa tunaweza kuchagua mbinu za kukabiliana navyo. Na ni katika kuzitafuta mbinu za kukabiliana na hali hizo ndio tunajikuta na maswali kama haya;

Je wewe kama mjasiriamali una security katika shughuli zako?
Je security yako ni ya namna gani? Na inakidhi matakwa ya Dunia ya sasa?
Je kitatokea nini katika maisha yako pale utakapopoteza uwezo wa kuzalisha mali, iwe ni kwa kutokana na uzee au ajali?


Ikumbukwe kuwa, moja ya sababu kuu inayomfungamanisha mfanyakazi na ajira yake ni security ya ajira hiyo. Ni security hiyo ambayo inamuhakikishia mfanyakazi uhakika wa maisha yake, kitu ambacho kinaweza hata kumkosesha ujasiri wa wakuiacha ajira hiyo na kujiajiri mwenyewe. Sasa Je, mjasiriamali naye anaweza kuwa na security ya namna hiyo katika shughuli zake?
 
Uzoefu wetu unaonyesha kuwa wajasiriamali wengi waliokuwa na biashara ndogo ndogo walizokuwa wakiziendesha wenyewe (owner operated business) wanaishi maisha ya kubahatisha sana baada ya kushindwa kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali kutokana na uzee au hali zao za kiafya

Je ni nani kati yetu angependa kuishi maisha ya kubahatisha baada ya kushindwa kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali hasa ukizingatia kuwa sehemu kubwa ya nguvu zake, sehemu kubwa ya maisha yake na sehemu kubwa ya ujana wake aliutumia katika namna ambayo haitakuja kumsaidia katika sehemu kubwa ya Uzee wake?

Watu wengi hawapendi kuzungumzia suala hili, hawapendi hata namna linavyozungumzika lakini ni dhahiri kuwa wale watakaojiandaa sasa ndio watakaofurahia maisha yao mbeleni kwani wanafursa ya kujipanga mapema. Malcolm X alipata kusema the future belongs to those who prepare for it today
 
Mkuu nenda moja kwa Moj najua hapa kinacho fuata utatoa Namba za simu an then utawaambi watu wakutafute au wahuhudhurie Semina ukumbi fulani, Hapa najua ni ishu za Forever Living tatizo unajaribu kuvuta watu
 
Mkuu nenda moja kwa Moj najua hapa kinacho fuata utatoa Namba za simu an then utawaambi watu wakutafute au wahuhudhurie Semina ukumbi fulani, Hapa najua ni ishu za Forever Living tatizo unajaribu kuvuta watu

Mdau,
Muungwana huwa anahoji pale asipokuwa na uhakika na taarifa ili asije akapotoka au akapotosha watu wengine kwa kutoa hitimisho lisilo sahihi. Sisii kama SEN tunaamin unakidhi vigezo vyote vya uungwana, lakin katika hili tuna haki ya kudhani kuwa umepotoka kidogo.

Ndugu, maudhui ya mjadala huu, yamejikita katika mbinu zinazoweza kutumiwa na wajasiriamali katika kujiwekea akiba ya uzeeni kuanzia sasa wanapokuwa wanafanya shughuli zao iwe ni hiyo ya network marketing, kilimo, ufundi au yoyote ile ili waweze kuishi maisha ya amani na furaha wakati wa uzee wao.

Wapo baadhi yetu wanajiwekea akiba zao za uzeeni katika mifumo isiyo rasmi, mfano kujenga nyumba za kupangisha ili wakati wakiishiwa uwezo wa kuzalisha kipato wawe wanaishi kutokana na kodi watakazopokea kutoka kwa wapangaji wao, mpango ambao ni mwema,

Wengine wanajiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii katika mpango wa hiari wa kujiwekea akiba ya uzeeni (voluntary savings retirement scheme) ili atakapofikisha umri wa kustaafu katika shughuli zake au kupoteza uwezo wa kuzalisha kipato aweze kupokea malipo ya uzeeni au mafao mengineyo.

Lakini wengi wetu, hatujiwekei akiba yoyote, na wala hatuna Exit Strategy katika biashara zetu, sasa swali ni je kama wewe ni mjasiriamali upo kundi lipi? Na umejianda vipi na maisha yako baada ya kupoteza uwezo wako wa kuzalisha kipato?

Angalizo
SEN (Songambele Entrepreneurial Network) ni taasisi ya kijasiriamali kwa ajili ya wajasiriamali na inaendeshwa na wanachama wake ambao ni wajasiriamali na wataalamu waliobobea katika sekta mbali mbali.

Moja ya huduma ambazo huwa tunazitoa pamoja na huduma nyingine ni business skills training, ambazo hata hivyo hutolewa kwa wanachama wetu tu. Hatuna ufungamanisho na Network Marketing Company yoyote hapa Afrika mashariki wala kwingineko ( japo hatuwakatazi wanachama wetu kuwa na ufungamanisho wa namna hiyo na kampuni hizo)

Unaweza ukatupata twitter kupitia link hii http://twitter.com/SongambeleEN
Usisite kututembelea na kutu-follow ikibidi
Asante
 
Mkuu so nyie mnatoa hiyo Huduma? mimi nijuavyo saving inawezwa kuwekwa kwa aina nyingi sana, ziwe rasimu au zisiwe rasim bado ni saving na saving si razima ziwe zilizo letwa n wazungu ndo zionekane zinafaa,
 
Mkuu so nyie mnatoa hiyo Huduma? mimi nijuavyo saving inawezwa kuwekwa kwa aina nyingi sana, ziwe rasimu au zisiwe rasim bado ni saving na saving si razima ziwe zilizo letwa n wazungu ndo zionekane zinafaa,

Mdau
Michango yako inaheshimika sana hapa jamvini.
Sisi kama SEN hatuna ufungamanisho na Pension Scheme yoyote, wala hatuna mamlaka ya kupokea fedha kama akiba kutoka kwa mtu yeyote, (hata kutoka kwa mwanachama wetu).

Tunachokifanya hapa ni kuchokoza mada tu, kwani kwa uzoefu wetu, tumekutana nayo haya huko kwenye shughuli zetu tukaona si vibaya tukiwashirikisha wadau kama ninyi, ili wajasiriamali wengi waweze kuelimika na kuchukua hatua sasa (kwa wale ambao bado hawajachukua hatua)

Hakuna sehemu yoyote tuliyosema kuwa mifumo iliyopendekezwa na wazungu ndio mifumo bora zaidi ya mifumo yetu mingine isiyo rasmi, na katika hili naomba tukiri kuwa wale waliofanikiwa kuwekeza akiba zao katika ujenzi wa nyumba za kupangisha wanapata faida kubwa sana (hii ni kutokana na uzoefu wetu) lakini ukweli huu haupaswi kutuzuia kufikiri juu ya hatma ya wale wasio na uwezo wa kufanya uwekezaji wa namna hiyo.

Katika hili tumalize kwa kusema amebarikiwa yule ambaye sehemu kubwa ya ujana wake anautumia katika namna ambayo itakuja kumsaidia katika sehem kubwa ya Uzee wake. Waswahili wanasema fainali uzeeni, lakin sisi tunasema mechi za kufuzu ni sasa, Tujiwekee akiba, kwa namna yoyote ile.

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…