Mjamzito adaiwa kuwanywesha sumu wanawe wawili, wafariki dunia

Mjamzito adaiwa kuwanywesha sumu wanawe wawili, wafariki dunia

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Watoto wawili wamefariki dunia na mmoja kunusurika kifo, baada ya mama yao mzazi kuwapa sumu ambayo ni dawa aina ya Tiktik ya kuoshea mifugo, kisha na yeye kunywa.

Akizungumza leo Jumanne, Novemba 22,2022, Kamada wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Filemon Makungu amesema tukio hilo limetokea Novemba 20, 2022 saa tatu usiku, mtaa wa Shede, Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Kamanda Makungu amesema mwanamke huyo Christina Akoonay (36), alikutwa amejifungia ndani ya nyumba anayoishi akiwa na watoto wake watatu hajitambui huku mtoto mmoja Daniel Deogratius (5),akiwa tayari amefariki dunia.

Kamanda Makungu amesema mwanamke huyo pamoja na watoto wake walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni, kwaajili ya kupatiwa matibabu na wakati wakiendelea na matibabu mtoto mwingine David Deogratias (1), alifariki dunia.

Kamanda Makungu amesema mtoto aliyebakia ni Davina Deogratias ((7) na mama yake ambao wanaendelea na matibabu hospitalini hapo na kwamba jeshi hilo linamshikilia mwanamke huyo kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni, Dk Stanley Binagi amethibitisha kuwepo kwa vifo hivyo akisema familia hiyo ilikunywa sumu ambayo ni dawa ya kuua wadudu kwenye mifugona mimea inayoitwa Tiktik.

Binagi amesema mwanamke huyo amekunywa sumu hiyo akiwa ni mjamzito na kwamba sumu hiyo haijaweza kumuathiri mtoto aliyeko tumboni na hali yake imeanza kuwa nzuri baada ya kuzimia kwa muda mrefu akiwa hospitalini hapo.

MWANANCHI
 
Kuna kesi kama hii kwa waliosoma sheria, Mama aliua watoto wake baada ya kuona watateseka sana bila Matunzo! Sikumbuki facts zake vizuri
 
Mmh ngumu kumeza basi angewatupa kanisan...sio kwa uchungu wanaopata kina mama leba
 
Itakuwa kama hii

 
Ni wabishi sana, wanasema kila mtoto anakuja na sahani yake.
Pia elimu ya uzazi wa mpango ni tatizo kubwa kwa wengi, wengi wanazaa bila kutaka.
Maisha magumu ila bado mnazaa. Anyway, sleep in peace toto’s
 
Kuna kesi kama hii kwa waliosoma sheria, Mama aliua watoto wake baada ya kuona watateseka sana bila Matunzo! Sikumbuki facts zake vizuri
Mama yake Taji liundi.
 
Yake ya familia ya Liundi yanajirudia? Madingi tuwe responsible na familia zetu aseee
 
Back
Top Bottom