KWELI Mjamzito anashauriwa anapotaka kung'oa jino afanyiwe wiki ya 13 - 28 ya ujauzito

KWELI Mjamzito anashauriwa anapotaka kung'oa jino afanyiwe wiki ya 13 - 28 ya ujauzito

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Wakuu

Nimemsikia mtu anahofia kung'oa jino ingawa anadai linamuuma sana ila anaogopa ujauzito wake unaweza ukaharibika.

Je, hii imekaaje wakuu?
1764655826496.png
 
Tunachokijua
Kung’olewa jino ni utaratibu wa kuondoa jino kutoka kwenye mfupa wa taya ya juu (maxillary) au taya ya chini (mandibular) pamoja na soketi ya fizi. Kwa kawaida hufanywa na daktari wa meno wa kawaida, daktari bingwa wa upasuaji wa kinywa (oral surgeon), au daktari bingwa wa magonjwa ya fizi (periodontist).

Je, ni salama kwa mjamzito kungo'olewa jino?

Tovuti ya Colgate kupitia makala yake ya "Is A Tooth Extraction during pregnancy safe?" wanabainisha kuwa kutoa meno wakati wa ujauzito ni salama.

Ingawa ni salama kung'oa meno kipindi cha ujauzito lakini kuna muda maalum unaoshauriwa wakufanya hivyo kulingana na uharaka wa tukio husika.

Inashauriwa muda mzuri wa kufanya matibabu ya meno katika robo ya pili kuanzia wiki ya 13 hadi 28, kwa sababu kuanzia wiki ya 28 hadi siku ya kujifungua inaweza kuwa ngumu sana kwa mjamzito kulala chali kwa muda mrefu.

Ingawa kama utahitaji matibabu ya dharura ikiwemo root canal ama kung'oa meno unaweza kufanya hivyo bila kujali muda wa ujauzito ulio nao ili kuondokana na maambukizi yanayoweza kutokea kwenye kinywa.

Tovuti ya healthline inaelza kuwa kama utapitia hali hizi unaweza kung'oa meno hata kama una ujauzito;
  • Unapata maumivu makali yanayoathiri maisha yako ya kila siku.
  • Kuna hatari ya kupata maambukizi.
  • Kuna hatari ya uharibifu wa kudumu kwa meno au fizi.
Matibabu yasiyo ya dharura, kama kuchunguza au kuboresha rangi ya meno (teeth whitening) na taratibu nyingine za urembo, yanapaswa kuahirishwa hadi baada ya kujifungua. Ni bora kuepuka aina hizi za matibabu wakati wa ujauzito ili kuepusha mtoto anayekua na hatari yoyote, hata kama ni ndogo.

JamiiCheck imewasiliana pia na Daktari wa Meno kutokea Dar es salaam, Dkt Majaliwa Mzungu anabainisha kuwa;

Haitakiwi kumng’oa jino mjamzito katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na miezi mitatu kabla ya kujifungua.

Sababu ni kwamba dawa zinazotumika wakati wa mchakato zinaweza kuathiri kiumbe kilichopo ndani ya tumbo la mjamzito.

Vitu kama ganzi au dawa zinaweza kusababisha mimba kuharibika wakati wa mwanzoni mwa ujauzito pia zinaweza kusababisha ajifungue kabla ya muda ikiwa vitatumika kuekea kujifungua.

Dkt. Majaliwa anaendelea kubainisha kuwa Kitendo hicho kinaweza kuwa na uhusiano na kuharibika kwa mimba kutokana na sababu zilizoanishwa hapo juu.
Back
Top Bottom