Kwa hali yangu hii ya ujauzito, leo nimeamka na hamu kubwa ya kula vitumbua.
Nimepita kwa mama mchoma vitumbua (vizuri sana), nimemsalimia, hakuitikia, nikaona isiwe shida. Kwa kuwa najua bei ya vitumbua ni Tshs.200/= kwa kitumbua kimoja sikuwa na haja ya kuuliza bei bali nikamwambia anipatie vitumbua viwili (2), akanijibu tena bila kuniangalia usoni, "S I U Z I". Nikabaki mdomo wazi, kwa pembeni alikuwepo kijana akanionea huruma, akaniambia kuwa hivyo vitumbua vyote nimevinunua napeleka hotelini. Nikamwambia basi niuzie kwa bei ya hotelini, akakubali akaniuzia vitumbua 2 kwa Tshs.1,000/=.
Hivi wafanya biashara ndogondogo wa jiji letu hili la Mongela kwanini mnakuwa na lugha ambayo haina mvuto kwa mteja? Nimebaini hilo tatizo siku nyingi, watu wa huku akiona biashara yake imeshamiri anakuwa na kiburi kwa wateja, hawajui kumshikilia mteja mpaka point ya mwisho.
Elimu ya Ujasiriamali hasa kipengele cha kutafuta masomo, kubuni mradi, kumhudumia mteja ni muhimu sana kwa watu hawa.
Hii habari nitaiendeleza baadae ngoja kwanza nimuone Dr. anipime mapigo ya mtoto wangu tumboni.