Mjane amegoma kurithiwa na shemeji yake!

Mjane amegoma kurithiwa na shemeji yake!

Curtis De Mi Amor

Senior Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
136
Reaction score
514
Mjane mmoja huku kitaa aliyefiwa na mumuwe na kuachiwa mi mali yakushiba ikiwemo mi jumba ya kifayari, mindinga ya maana na ma maduka ya ujazo yote amegoma kurithiwa na shemeji yake.

Shemeji mtu ni kaka wa marehemu hivo alitaka amrithi huyo mjane ili mali zisiende mbali na nyumbani.

Sasa huyo mjane amegoma na anataka alete boya wake ndio waishi naye.

Je, ni haki kweli?

Kwanini agome kurithiwa?
 
Kurithiwa kulishapitwa na wakati, kumleta Mwanaume kwenye hiyo Nyumba ni marufuku labda wakaishi sehemu nyingine hapo wabaki Watoto.
Matrimonial home ni nyumba ya mke na mume, mume akifa mke anahaki ya kuleta mwanaume mwengine kama ambavyo mwanaume ana haki hiyo mke akifa. Lakini kwenye angle ya kimaadili nakubaliana na wewe.
 
Yeah,ndivyo inavyopaswa.Umepata Mpenz akupeleke kwake siyo umlete Kwenye nyumba ya marehemu.Tunakosea sana
Ni kukosa adabu na heshima kwa mumewe alie tangulia hata familia kwa ujumla. Nae huyo mwanaume anae enda hapo kuishi hana akili ana mavi kichwani ni kipimo tosha huyo jamaa ni bomu sasa wamekutana wote machizi
 
Wapuuzi hao wanaoleta mila za kitapeli.

Mnaotokwa mapovu je huyo shemeji anaetaka kurithi akikubaliwa bila aibu nae ataenda kulala kwenye kitanda alicholala ndugu yake?kunya anye kuku akinya bata kaharisha mxieeewwww

Mjane yupo huru kuishi atakavyo
 
Mbinu ni kupangisha kisha yeye akapange nyumba nyingine ili aishi na bwana wake
Huyo mwanamke malaya malaya tu, wajane ambao walikuwa waaminifu na kuwapenda waume zao haswaa, huwezi kuta anaolewa tena au kuwa na mwaume mwingine. Huyo malaya huenda hata alikuwa ana mcheat mume wake kipindi yupo hai na huyo mwanaume wake mpya
 
Back
Top Bottom