Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mjane wa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Shinyanga, Mariam Mongi (86), ambaye ni mmoja wa wamiliki wa eneo lenye ukubwa wa ekari 10 lililopo Madale, Mtaa wa Scout, Wilaya ya Kinondoni, amesema alikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa siku mbili kufuatia amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.
Mongi amesema alikamatwa Septemba 19, 2026 baada ya Mkuu wa Mkoa huyo kufika eneo hilo kufuatia mgogoro wa ardhi unaohusisha familia yake na wakazi waliodaiwa kujenga na kuishi katika eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Septemba 23, 2026, baada ya kutoka mahabusu, Mongi amesema Mkuu wa Mkoa alifika eneo hilo kwa ajili ya mkutano uliokuwa ukihusisha familia ya wamiliki wa ardhi na wakazi waliokuwa wamejenga katika eneo hilo, lakini familia yake haikufika.
Amesema baadaye aliona agizo la Mkuu wa Mkoa likiielekeza familia yake kukamatwa kwa madai ya kutotii wito wa kufika katika eneo la mkutano, akisisitiza kuwa familia yao haikupokea taarifa yoyote rasmi kuhusu wito huo.
Mongi amesema familia yao haikujulishwa kuhusu mkutano huo wala haikupokea wito wa kufika eneo la mgogoro kabla ya hatua ya kukamatwa kuchukuliwa.