Mjane wa Mongi, simulia alivyokamatwa na kukaa rumande kwa siku mbili kwa amri ya RC Chalamila

Mmh maisha haya aisee huyo mbibi wa kumweka ndani kweli si kutafuta laana za maisha hizo..
Hakuna cha laana. Wanafanya manipulation na kutafuta sympathy kwa jamii. Oda ilitoka wakamatwe wawekwe ndani. Askari walipokuja wakabeba wote ikiwemo huyo bibi.
Hiyo familia wamefanya ushenzi kwa kaya za watu kule Madale kwenye eneo wanalodai lao. Hawakuwa na busara na walikaidi amri ya kuitwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
 
Kuwaweka ndani ndio kutatua tatizo au sema bongo mnaoneana sana aisee..
 
Kila mtu ana mamlaka yake sehemu ya kazi
Mkuu wa Polisi hakuweza kuhoji kwanini amfunge bibi huyu?
Basi hata angemuweka tu sehemu badala ya kumtupa lockup
Kwa kweli wote watalipa hapa hapa duniani
 
Hakuna uonevu. Wao wamekaidi amri na zaidi wamewavunjia watu na kuharibu samani. Unaona walichofanya ni sawa?
samahni wewe ni dr wa nini? mbona unayo andika hayaendani na iyo title
Hakuna uonevu. Wao wamekaidi amri na zaidi wamewavunjia watu na kuharibu samani. Unaona walichofanya ni sawa?
sheria ipi inasema ukiitwa na mkuu wa mkoa usipo enda uwekwe ndani? kuhusu kuvunja nyumba ni amri ya mahakama wao sio tatizo lao wa haki na hiyo sehemu tufike mahali tuwe tunaheshimu vitu vya watu hasa ardhi haya mambo sikia kwa wengine usiombe yakukute wewe sisi kuna kesi ya kiwanja bahari beach mtu kavamia anasema chake aliuziwa na mwenye nacho na kashirikiana na watu wa ardhi kufoji baadhi ya nyaraka kesi tumekaanayo mahakamani zaidi ya miaka tisa mwezi uliopita ndio hukumu imetoka kuwa sisi ndio tuna haki sasa kwa mazingira hayo mtu hata kama kajenga mmiliki halali sio shida zake utabomoa tu
 
Samahani, jifunze kwanza kuandika. Makosa mengi ya kisarufi na kimuundo. Kuwekwa ndani unajua ni kwa sababu gani wamewekwa ndani? Huna unachojua.
 
Jinai haina umri
 
Hebu fafanua zaidi hii.
 
Hebu fafanua zaidi hii.
Inasemekana hii familia ilipokea wito wa mkuu wa mkoa lakini wakaleta kiburi wakagoma kwenda.
Ni hivi walitakiwa wakakae kikao Cha maridhiano kati Yao na waliojenga juu ya eneo lao ambao waliuziwa na mtu mwingine na wao hawana kosa,Kwa kifupi hawahusiki na huo mgogoro.
Maridhiano ni kwamba zile familia zote zilizojenga juu ya eneo lao ziwalipe viwanja walivyokatiwa Kwa bei ya Sasa
Mfano ulinunua mwaka 2020 Kwa mil 20.sasa hivi utailipa Tena hii familia mfano bei ya Sasa mil 35.yaani unanunua mara mbili.
Maana ni hasara hiyo familia kuporomosha nyumba za bei ghali mtaa mzima ili tu wahodhi Tena kiwanja chao huku hawa wakazi wanaenda kuanza Moja,watafute kiwanja bado waanze kujenga upya.hapa busara Kwa pande zote ilihitajika.
 
Oooh hapo sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…