Bibi wa kufikia na Babu yetu walikubaliana kwamba asije hapo kwa kutamani kurithi mali laah hasha bali ni kumtunza yeye kwa upendo tu na kama endapo atafariki basi ataridhi vitu vilivyomo chumbani kwake tu (Yaani chumbani kwa Babu yetu)
Bibi alikubali masharti ambayo hayakuandikwa popote na maisha ya kumlea mzee mwenake yakaanza - sisi wajukuu tukampenda bibi yetu mpya sababu alikuwa na roho nzuri ya utu.
Sasa Babu alipofariki, wakati balaza la ukoo linaendelea aliombwa Bibi aseme chochote kilichomo rohoni mwake - akafunguka akasema walikubaliana na marehemu kwamba hatarithi chochote isipokuwa vitu vilivyomo chumbani kwa marehemu tu kwa roho nyeupe kabisa.
Familia ikaafiki, ila wakaamua kumpatia nyumba nzima na mashamba kwa masharti asirisishe wala kuyauza !! akishaondoka itabakia mali ya familia.
Upo kiongozi? hapo ukatili upo wapi? Tunataka wajane wote wanaowaoa wazee ambao afya zao haziko sawa waige mfano wa Bibi yetu kipenzi.