Mjema asisitiza elimu ya kutunza mazingira kwa wananchi ili kukwepa majanga

Mjema asisitiza elimu ya kutunza mazingira kwa wananchi ili kukwepa majanga

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
MJEMA ASISITIZA ELIMU YA KUTUNZA MAZINGIRA KWA WANANCHI ILI KUKWEPA JANGWA, UKAME NA MMOMONYOKO WA ARDHI.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Sophia Edward Mjema ameitaka Serikali kupitia kwa maafisa wake wa kilimo na maafisa mazingira kutoka maofisi na kwenda kwa wananchi kuwaelimisha namna bora ya kulima ili wasijiingize kwenye kilimo kinachoweza kusababisha jangwa, ukame na mmomonyoko wa ardhi.

Mjema ameyasema hayo kwenye mwendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo kwenye wilaya ya Kiteto mkoani Manyara ambapo amesisitiza sana kilimo bora kinachofuata misingi bora ya ulimaji kwa wananchi.

"Ndugu zangu mnaona jua lilivyo kali, miti imekatwa sana hapa na ardhi kule juu kwenye milima mnalima tena mnalima kilimo cha kuparua ambacho kinafanya kule juu ardhi inaachia na kusababisha mmomonyoko ambao ni hatari." Alisema na kuongeza

"Miti ikipandwa inashikilia ardhi vyema na hata mvua ya namna gani ikija haiwezi kuporomosha udongo lakini mkiendelea na kilimo cha mlimani cha kuparua ardhi mnateremsha udongo, kunakuwa na mmomonyoko na udongo ukianguka utaua watu huku chini na kuliweka eneo hili kwenye hatari ya jangwa." Alisisitiza Mjema akiwataka wakulima kuzingatia kilimo bora.

Mwenezi Mjema akawataka maafisa wa Serikali hasa wa kilimo na mazingira kupita kata kwa kata kuangalia aina ya kilimo wanachofanya wananchi kwenye maeneo hayo na wao kama Watalaamu watoe elimu juu ya kilimo wanachopaswa kulima kwenye maeneo ya milima na maeneo yao pamoja aina ya miti ya kupanda kushikilia ardhi ili kuepusha majanga ya mmomonyoko wa udongo, ukame na jangwa.

Mjema aliambatana na Katibu Mkuu wa CCM kwenye ziara yake hiyo mkoani Manyara ambayo ilijikita kusikiliza na kutatua kero za wananchi, kuimarisha Chama na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
IMG-20230311-WA0004.jpg
IMG-20230311-WA0003.jpg

 
Back
Top Bottom