Mjema awakumbuka wasiojiweza na wenye mahitaji Dar

Mjema awakumbuka wasiojiweza na wenye mahitaji Dar

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Edward Mjema Alhamisi Aprili 06, 2023 ametoa futari kwa watu na makundi mbalimbali kwenye Jamii kwenye mwendelezo wa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan.

Mwenezi Mjema kwenye ujumbe wake ameeleza:-

"Tukiwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Leo Jijini Dar es Salaam kupitia ofisi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, tumeweza kutoa FUTARI kwa makundi mbalimbali yakiwemo yale yenye uhitaji.

Kipekee nimshukuru Camel Oil kwa kufanikisha zoezi hili na kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Tuutumie mfungo huu, kwa kuendelea kuliombea taifa letu na Viongozi wetu mbalimbali wa Chama na Serikali."

#RamadhanKareem
#VitendoVinaSauti
#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom