Mjema: Serikali awamu ya sita imedhamiria kuboresha huduma ya mama na mtoto Tanzania

Mjema: Serikali awamu ya sita imedhamiria kuboresha huduma ya mama na mtoto Tanzania

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029
IMG-20230204-WA0173.jpg

SOPHIA MJEMA:SERIKALI AWAMU YA SITA IMEDHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO.

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesisitiza moja ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha huduma za afya hasa ya Mama na Mtoto inaendelea kuboreshwa ili wapate huduma zilizo bora zinazoambatana na vifaa tiba vya kisasa.

IMG-20230204-WA0179.jpg
Akizungumza leo Februari 4,2023 na wananchi wa Mikese baada ya kufanya ziara katika Kituo cha Afya Mikise mkoani Morogoro , Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Itikadi na Uenezi Sophia Mjema amesema lengo mojawapo la Serikali ya Chama hicho ni kuboresha huduma za afya kwa kutoa huduma bora na vifaa tiba vilivyobora.

“Katika Kituo cha Afya Mikese tumeona jengo la Mama na Mtoto lakini tumeona vifaa tiba ambavyo ni bora na vya kisasa kabisa kikiwemo kitanda cha kujifungulia , akina mama mnajua ukishapata uchungu unakaa unahangaika hangaika lakini kitanda chenyewe kinakwambia geuka kulia, geuka kushoto , kwa hiyo wanawake wanajifungua kwa raha.

“Yote hayo yanafanyika kwa sababu ya Rais Samia Suluhu Hassan lakini kwa namna ambavyo Serikali imeamua kuboresha huduma za mama na mtoto baada ya mama kujifungua anakwenda kwenye eneo maalum kwa ajili ya kuangalia afya zao kama ziko vizuri lakini hata akienda nyumbani bado kuna utaratibu wa kufuatilia ili kujua maendeleo. Yote hayo yanafanyika chini ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),”amesema Mjema.

Ameongeza Serikali ya Awamu ya Sita inataka kuona mama anajifungua vizuri na aendelee kukuwa akiwa na akili zake vizuri huku akitumia nafasi hiyo kukumbusha wazazi kuzingatia siku 1000 katika kumlea mtoto ikiwa pamoja na kunyonyweshwa vizuri na kulishwa vizuri na kupata virutubisho.

“Mtoto akitoka hapo hao ndio wanakuwa ma-genius(vipaji) wa baadae kwa hiyo akina baba , akina mama tuhakikishe tunasomesha watoto wetu lakini tunahakikisha tunamsomea mtoto wa kike vizuri zaidi ,mtoto wa kike ana kumbuka nyumbani , kwa hiyo haya yote yanayofanyika katika huduma za afya ni kwa ajili ya kuhakikisha tunamsaidia mama anayeleta binadamu mwingine kwenye dunia hii

“Lakini katika kuhakikisha binadamu huyo anakuwa vizuri ni jambo la kuweka mikakati kwamba binadamu huyu anayezaliwa Tanzania azaliwe vizuri, alelewe vizuri kwenye zile sikue 1000 zake na apate lishe nzuri baada ya hapo atakapokuwa ndipo tutakuwa na watu wenye akili watakaotoka hapa Tanzania.

“Ili tufike huko lazima kuwepo na mikakati ikiwemo ya kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.Mama Samia ni mama mikakati na anaona mbali na anajua akikutayarisha hivi baadae nchi itakuwa inaongoza Afrika lakini duniani , tunataka tukimbie twende katika nchi ambazo zimeendelea zaidi,”amesema Mjema.

IMG-20230204-WA0172.jpg
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu) pamoja na Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali ambapo ziara hii ina lengo la Kukagua, Kuhimiza na Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025
 
Hivi ni kweli kwamba mama na mtoto wanatibiwa bure au ndio mambo ya kudanganyana....hii siamini . nenda hospitali ukaone /usikie wanachokwambia .watakwandikia dawa ujanunua .waulize wenye bima watawaelewesheni .sisemi sana.....
 
Hivi ni kweli kwamba mama na mtoto wanatibiwa bure au ndio mambo ya kudanganyana....hii siamini . nenda hospitali ukaone /usikie wanachokwambia .watakwandikia dawa ujanunua .waulize wenye bima watawaelewesheni .sisemi sana.....
Unachotakiwa kufanya ni kuripoti tu kama umetozwa fedha,
 
Unachotakiwa kufanya ni kuripoti tu kama umetozwa fedha,
IMG_20230204_225029.jpg
IMG_20230204_224942.jpg
dogo ana kitu kinawasha kifuani hospitali wameandika dawa hii .ana mwaka 1.. ndiyo maana makataa hii kauli yenu ya mama na mtoto
 
Unakwenda kuripoti kwa nani wewe mzee? Kama wanakwamisha dawa hamna . unataka kuripoti wapi badala ya kuondoka.utapoteza mda wako bure
 
Nenda kwa Mkurugenzi
Tatizo kubwa la MaCCM MACHAWA mnabweka bweka tu Wala hamjui taratibu na mifumo mingi inavyofanya kazi.

Hao Wakurugenzi ndio WANALALA WANAOTA MAPATO.

Hata siku moja DED hawezi kukusikiliza eti una mtoto au mzee umelipishwa dawa au matibabu.

Unless Kama mtu kalipia halafu pesa imepigwa.
 
Back
Top Bottom