Mpandafarasi
Member
- Dec 7, 2008
- 57
- 11
Mjeshi aliyemchapa Trafiki,anyea debe!
Jeshi letu la Wannanchi (JWTZ), limenasa na kumtupa lupango Koplo Steven Sagana, kwa kuhusika na kosa la kuongoza kichapo kwa askari wa Usalama Barabarani, Sajini Thomas, juzi Dsm.
Koplo Sagana na wenzake walitenda shambulio hilo la kikatili kwenye mataa ya Ubungo...ambapo ni makutano ya barabara za Morogoro, Mandela....kwa madai ya kucheleweshwa na Trafiki huyo aliyekuwa akiongoza magari katika eneo.
Taarifa ilidodonshwa kwa vyombo vya mijinews na Kurugenzi ya Habari ya jesho hilo,ilisema kuwa jeshi hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini limeunda timu ya pamoja kuchunguza na kubaini undani wa mazingira ya tukio hilo ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wote waliohusika.
Hatua za awali za kinidhamu zilizochukuliwa na JWTZ kufuatia tukio hilo baya ni pamoja na kumkamata na kumburuza ndani Koplo Steven Sagana wakati wakibainishwa wenzake waliohusika na tukio hilo, ilisema taarifa ya JWTZ ambayo ilieleza kusikitishwa na kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na askari wake.
Tunapenda kuwahakikishia wananchi kuwa JWTZ itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti nidhamu ya wanajeshi wote, kuimarisha ushirikiano na vyombo vyote pamoja na wananchi kwa ujumla sambamba na kuwa tayari wakati wote kutekeleza jukumu la ulinzi wa taifa letu pamoja na majukumu mengine mbalimbali, iliongeza taarifa ya Jeshi hilo.
Source: Darhotwire.com