Paschal Ruta
Member
- Jul 16, 2016
- 42
- 27
- Thread starter
-
- #21
Nadhani kila mji una vipaji vyake...hakuna haja ya kusafiri kwenda mji mwingine
Ningekuwa na mamlaka husika ningechagua mji mmoja ambao ungejengewa miundo mbinu mbalimbali halafu wadau mbalimbali wa sanaa wakapewa motisha ya kuwekeza sehemu hiyo.
Katika mji huo kutakuwa na studio mbalimbali za production, studio za muziki, makampuni ya usaili wa wasanii, makampuni ya kuuza na kukodisha vifaa, vituo vya mafunzo, nk.
Kwa mtazamo wako unadhani mji gani ungefaa kwa jukumu hili? Inabidi kuzingatia mandhari ya eneo, hali ya hewa, mahali mji ulipo na ukaribu wake na miji mingine ya kimkakati, nk.
Ukishawekeza kwenye mambo ya msingi, kutachochea ujenzi wa mahoteli, migahawa, kumbi za starehe, makazi bora, nk.
PS. Dar es salaam na Dodoma hapafai.
Huko Moro wawekewe huduma ya maji safi kwanza,ndio entertainment ifuate.
Na Suzane CheddyKuna Sehemu Ina maji Safi Kama Morogoro...!
Pure natural water from Uruguru mountains, Udzungwa highlands, NK.
We jamaa yangu inaijua Morogoro kweli.
Au ulimaanisha maji ya Bakhresa kuwa hayapo Morogoro.
Yah kweli mbona wenzetu wametenga mji ya sanaa mfano marekani kila mji una matumizi yake sehemu za starehe unaenda Miami, sehemu ya maofisi ya serikali unaenda Washington Dc, sehemu ya wanakamari wanaenda Las Vegas. Sanaa unaenda Calfornia
Kule Calfornia ndio sehemu ambapo studio kubwa kama hollywood zipo humo, michezo ya watoto theme parks zipo humo. Yani kuweka kila mji na specific zake. Yani bagamoyo ilifaa sana kwa sanaa, kuanzia hali ya hewa mandhari yake yani just perfect...!!! Makampuni ya sanaa yangekuwaga kule yani safi sana huku kwingine kuwe sehemu tu za location nn basi