Mji gani unafaa kuwa Center ya Sanaa Tanzania?

Mji gani unafaa kuwa Center ya Sanaa Tanzania?

Nadhani kila mji una vipaji vyake...hakuna haja ya kusafiri kwenda mji mwingine

Bado hakutazuia makampuni mengine kufanya biashara hizo miji mengine.

Hoja yangu ni kuwa na center ya sanaa na kazi zingine za ubunifu. Ukielewa hoja yangu utaelewa faida na mantiki yake.
 
Ningekuwa na mamlaka husika ningechagua mji mmoja ambao ungejengewa miundo mbinu mbalimbali halafu wadau mbalimbali wa sanaa wakapewa motisha ya kuwekeza sehemu hiyo.

Katika mji huo kutakuwa na studio mbalimbali za production, studio za muziki, makampuni ya usaili wa wasanii, makampuni ya kuuza na kukodisha vifaa, vituo vya mafunzo, nk.

Kwa mtazamo wako unadhani mji gani ungefaa kwa jukumu hili? Inabidi kuzingatia mandhari ya eneo, hali ya hewa, mahali mji ulipo na ukaribu wake na miji mingine ya kimkakati, nk.

Ukishawekeza kwenye mambo ya msingi, kutachochea ujenzi wa mahoteli, migahawa, kumbi za starehe, makazi bora, nk.

PS. Dar es salaam na Dodoma hapafai.

Morogoro midway
 
Kuna Sehemu Ina maji Safi Kama Morogoro...!
Pure natural water from Uruguru mountains, Udzungwa highlands, NK.
We jamaa yangu inaijua Morogoro kweli.
Au ulimaanisha maji ya Bakhresa kuwa hayapo Morogoro.

Huko Moro wawekewe huduma ya maji safi kwanza,ndio entertainment ifuate.
 
Kuna Sehemu Ina maji Safi Kama Morogoro...!
Pure natural water from Uruguru mountains, Udzungwa highlands, NK.
We jamaa yangu inaijua Morogoro kweli.
Au ulimaanisha maji ya Bakhresa kuwa hayapo Morogoro.
Na Suzane Cheddy

Kutokana na maji kuwa sehemu kubwa ya maisha ya mwanadamu wananchi wa mtaa wa Mafisa uliopo ndani ya manispaa ya Morogoro wamelalamikia uongozi wamtaa kutokana na tatizo la uhaba wa maji wanaoupata kadiri siku zinavyoendelea.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wanakijiji kutokana na mgao wa maji unaendelea ambapo awali walikuwa wakipata maji kila baada ya siku tatu lakini kwa sasa wanapata maji baada ya wiki moja hadi nne hali inayopelekea kuhatarisha maisha yao.

Bi.Fatma Shaaban mkazi wa mtaa wa Mafisa amesema kuwa uongozi wao umekuwa ukitoa ahadi ya kumaliza mgogoro wa maji lakini hadi sasa hakuna mabadiliko yoyote na pia wamekuwa wakitumia maji yaliyotuama bondeni ambayo si salama kwa matumizi hivyo kusababisha magonjwa ya mlipuko.

Naye Alex Zuberi amesema kuwa mhusika wa kufungua maji katika mtaa amekuwa chanzo kikubwa cha tatizo kwani hufungua maji usiku wa saa tano na kuyafunga asubuhi hivyo kuhatarisha maisha ya wanakijiji na pia kutokidhi mahitaji ya maji kwa wananchi.

SUAMEDIA imezungumza na mwenyekiti wa mtaa wa Mafisa Bw.Nasoro Hamis Kapanda ambapo amesema tatizo la maji linatokana na bomba dogo lililofungwa eneo hilo na kukiri pia kuwa,mfungua maji wa eneo hilo kuwa na utaratibu mbovu wa kufungua maji.

Mwenyekiti huyo wa mtaa amesema amekuwa akipeleka malalamiko ya wananchi katika uongozi wa juu lakini hakuna majibu wala utekelezaji unaofanyika hivyo ameomba uongozi wa manispaa ya Morogoro kushughulikia tatizo hilo ili kuepusha mtaa wa Mafisa katika katari ya kukumbwa na maradhi ya mlipuko.
 
Naona wengi mnataja maeneo karibu na Dar. Vipi huu mradi ukifanyika sehemu kama Mwanza?
 
Yah kweli mbona wenzetu wametenga mji ya sanaa mfano marekani kila mji una matumizi yake sehemu za starehe unaenda Miami, sehemu ya maofisi ya serikali unaenda Washington Dc, sehemu ya wanakamari wanaenda Las Vegas. Sanaa unaenda Calfornia

Kule Calfornia ndio sehemu ambapo studio kubwa kama hollywood zipo humo, michezo ya watoto theme parks zipo humo. Yani kuweka kila mji na specific zake. Yani bagamoyo ilifaa sana kwa sanaa, kuanzia hali ya hewa mandhari yake yani just perfect...!!! Makampuni ya sanaa yangekuwaga kule yani safi sana huku kwingine kuwe sehemu tu za location nn basi
 
Umetisha sana mkuuu

Nichagulieni mji ili niweze kuwapa jibu
 
Back
Top Bottom