A
Anonymous
Guest
Mimi ni mkazi wa Mji Mdogo wa Ikwiriri uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani.
Mji wa Ikwiriri unakua kwa kasi na tayari una idadi kubwa ya wakazi, lakini cha kushangaza hadi sasa hauna machinjio rasmi ya mifugo kama ng’ombe, mbuzi na kondoo kwa ajili ya shughuli za wafanyabiashara wa nyama.
Kutokana na kukosekana kwa machinjio rasmi, wafanyabiashara wengi wa nyama wamekuwa wakichinjia mifugo katika maeneo yasiyo rasmi wanayoyajua wao. Hali hii imesababisha kuongezeka kwa mabucha bubu na uuzaji wa nyama za mitaani, ambazo baadhi zinadaiwa kutoka kwa mifugo waliokufa wenyewe au waliokuwa wagonjwa.
Pia kuna malalamiko kuwa maafisa husika, wakiwemo Afisa Afya na Afisa Mifugo, hawasimamii ipasavyo suala hili, hali inayohatarisha afya za wananchi kutokana na uwepo wa nyama zisizo salama.
Mbali na athari za kiafya, mabucha yasiyo rasmi yamekuwa yakileta ushindani usio sawa kwa wafanyabiashara wenye mabucha halali, kwani huuza nyama kwa bei ya chini kutokana na kutofuata taratibu zinazohitajika.
Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua kuhakikisha Mji wa Ikwiriri unapata machinjio rasmi na usimamizi wa kutosha ili kulinda afya za wananchi na kuimarisha biashara halali za nyama.