Katika maisha ya mwanadamu hakuna ukweli au uhalisia ambao mara nyingi watu wengi huwa tunajaribu kuukimbia kama kujua kuwa pamoja na uhalali wa mtu kumiliki na kutumia anachomiliki atakavyo bado tamaduni na sheria za jamii yake zinambana na anapaswa akubaliane nazo. Tabu ni pale unapotaka kuleta utamaduni wa kigeni au mpya katika jamii yako na kutaka kuifanya jamii nzima ikubaliane na takwa lako. Na hii inajidhihirisha katika maneno, shutuma na kuandamwa kwa mtu na jamii husika.
Ni kweli kuwa kiungo hicho ni mali yako, umepewa na Muumba wako bure, lakini je katika jamii uliyokuzwa nayo inakubalika kukitumia utakavyo au ni kinyume na matarajio ya jamii husika? ......Ukitaka kutumia uhuru huo tafuta jamii nyingine inayobariki matakwa yao.
Hizi lugha za ni mali yangu natumia nitakavyo ni kujifariji tu kwa muhusika na wala haijustify kuruhusiwa au uhuru wa kukitumia kwa style atakayo. Kauli za namna hii huwa hazina mashiko na wala hazijengi hoja na kama zingekuwa zinajenga hoja wangekuwaga wanaruhusiwa na wao wenyewe wangekuwa huru kufanya waziwazi bila wasiwasi wala kutumia nguvu nyingi kujustify matendo yao.