Mji wa Florida waondoa katazo la kuvaa 'mlegezo'

Mji wa Florida waondoa katazo la kuvaa 'mlegezo'

Faith Luvanga

Member
Joined
Aug 21, 2018
Posts
14
Reaction score
15
Baada ya miaka 13 mji wa florida nchini Marekani umeondoa katazo la kuvaa milegezo kwa jinsia zote ambayo ilikua inazuia watu kuvaa nguo zinazoonesha nguo za ndani.

Mamlaka ya mji wa Opa-loka ilipiga kura ili kurudisha sheria ya mwaka 2007 na agizo la 2013 lilikua linawataka wanaume na wanawake kutovaa nguo zinazoonesha nguo za ndani, ambapo waliounga mkono sheria hiyo kurudishwa waliwazidi waliokua wanapinga kwa kura 4 kwa moja.

Katika mji wa Florida ulioko kaskazini mashariki mwa mji wa Miami kuna vibao vinavyoonesha katazo hilo, ambapo kuna picha za vijana wawili wa kiume wakiwa wamevalia suruali chini ya viuno vyao, na kuna maneno yanayosomeka 'Hakuna utata tena..... Ni sheria!'

Meya wa Mji huo, Chris Davis,aliliambia gazeti la 'The Miami Herald' kuwa alikua hakubaliani kabisa na sheria hiyo hat anngekua raia wa kawaida na kuongeza kuwa sheria hiyo ilikua inakandamiza baadhi ya makundi ya watu jijini hapo ambao ni vijana wamarekani wenye asili ya kiafrika.
 
... hivi Florida ni mji/jiji? Sio jimbo lile? Nachojua Miami, Jacksonville, Orlando, n.k. ni miongoni mwa majiji katika Florida huku Tallahassee ukiwa mji mkuu.
 
Back
Top Bottom