Mji wa Kowloon Walled

Mji wa Kowloon Walled

Military Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2019
Posts
761
Reaction score
1,464
fd687e07c6428552d853aaff0f404662.jpeg
IMG_20200405_022441_187.jpeg

Kama unaijua au umewahi kuisikia Sodoma na Gomola, dhambi na ufuska uliokuwa ukifanywa katika kipindi hicho basi ndivyo ilivyokuwa katika mji wa Kowloon Walled City uliopo Hong Kong China kati ya mwaka 1898 hadi 1994. Kowloon Walled City maana yake mji wa Kowloon uliopo ndani ya uzio, ukuta.

Miaka ya nyuma hapa palikuwa ni kambi kubwa ya kijeshi ya wachina, baadae walivyonyang'anywa na wakoloni ukaja kuwa mji ambao ulikuwa ndani ya ukuta, mji wote ulizungushiwa ukuta mrefu kwakua mwanzo ilikuwa ni sehemu ya kijeshi, idadi ya wakazi katika mji huu ilifika 50,000.

Huku hakukuwa na kiongozi wa aina yoyote, hakukuwa na serikali, watu walikuwa huru kufanya lolote, ujambazi, uzinzi, ukahaba na kila aina ya ufuska ilikuwa inafanyika huku bila kujali, ilikuwa kama enzi za Sodoma na Gomola hadi baaadae mji huu ukaanza kuitwa 'Hak Nam' yaani Mji wa Giza.

Mji huu ulikuwa ndani ya uzio, ukuta mrefu sana kwenda juu, sheria zilikuwepo, lakini zilikuwa zinatekelezwa nje ya uzio na sio ndani ya uzio kulimo mji huu, yaani humo unaambiwa ni kama hakukuwa duniani vile, hakukuwa na shule wala hospitali, lilikuwa ni eneo la ekari 6 tuu, lakini kulikuwa na maghorofa makubwa watu kuishi.

Mwaka 1987 serikali ya China ilitangaza kuwahamisha wakazi wote kinguvu katika mji huu na kuubomoa kabisa mji wote, watu walikuwa wagumu kuhama lakini hadi kufika April 1994 mji ulikuwa hauna mtu yoyote anaeishi, zaidi ya askari 150 walipewa kazi ya kufukuza watu katika mji huo, na huo ndio ukawa mwisho wa uchafu wote uliokuwa ukifanywa huko.

Chanzo cha watu kupewa uhuru katika mji huu ni kipindi cha utawala wa Uingereza huko China, kulikuwa na makubaliano yaliyosainiwa mwaka 1898 kati ya China na Uingereza ili mtu yoyote katika mji huo aishi bila sheria yoyote, huko unaambiwa kumuona kahaba wa miaka 70 au 80 ilikuwa kawaida, ngono nje nje.

Hata wakati China inatangaza kuubomoa mji mzima mwaka 1987 pia ilibidi kwanza serikali ya Uingereza kupitia waziri mkuu Magreth Thatcher watie sign ili kuuvunja mkataba huo wa mwaka 1898, vinginevyo hadi leo ungekuwepo.

9a3dafb481b72788ca5ba03282efe885.jpeg

@military_Genius
 
View attachment 1409009View attachment 1409010

Kama unaijua au umewahi kuisikia Sodoma na Gomola, dhambi na ufuska uliokuwa ukifaanywa katika kipindi hicho basi ndivyo ilivyokuwa katika mji wa Kowloon Walled City uliopo Hong Kong China kati ya mwaka 1898 hadi 1994. Kowloon Walled City maana yake mji wa Kowloon uliopo ndani ya uzio, ukuta.

Miaka ya nyuma hapa palikuwa ni kambi kubwa ya kijeshi ya wachina, baadae walivyonyang'anywa na wakoloni ukaja kuwa mji ambao ulikuwa ndani ya ukuta, mji wote ulizungushiwa ukuta mrefu kwakua mwanzo ilikuwa ni sehemu ya kijeshi, idadi ya wakazi katika mji huu ilifika 50,000.

Huku hakukuwa na kiongozi wa aina yoyote, hakukuwa na serikali, watu walikuwa huru kufanya lolote, ujambazi, uzinzi, ukahaba na kila aina ya ufuska ilikuwa inafanyika huku bila kujali, ilikuwa kama enzi za Sodoma na Gomola hadi baaadae mji huu ukaanza kuitwa 'Hak Nam' yaani Mji wa Giza.

Mji huu ulikuwa ndani ya uzio, ukuta mrefu sana kwenda juu, sheria zilikuwepo, lakini zilikuwa zinatekelezwa nje ya uzio na sio ndani ya uzio kulimo mji huu, yaani humo unaambiwa ni kama hakukuwa duniani vile, hakukuwa na shule wala hospitali, lilikuwa ni eneo la ekari 6 tuu, lakini kulikuwa na maghorofa makubwa watu kuishi.

Mwaka 1987 serikali ya China ilitangaza kuwahamisha wakazi wote kinguvu katika mji huu na kuubomoa kabisa mji wote, watu walikuwa wagumu kuhama lakini hadi kufika April 1994 mji ulikuwa hauna mtu yoyote anaeishi, zaidi ya askari 150 walipewa kazi ya kufukuza watu katika mji huo, na huo ndio ukawa mwisho wa uchafu wote uliokuwa ukifanywa huko.

Chanzo cha watu kupewa uhuru katika mji huu ni kipindi cha utawala wa Uingereza huko China, kulikuwa na makubaliano yaliyosainiwa mwaka 1898 kati ya China na Uingereza ili mtu yoyote katika mji huo aishi bila sheria yoyote, huko unaambiwa kumuona kahaba wa miaka 70 au 80 ilikuwa kawaida, ngono nje nje.

Hata wakati China inatangaza kuubomoa mji mzima mwaka 1987 pia ilibidi kwanza serikali ya Uingereza kupitia waziri mkuu Magreth Thatcher watie sign ili kuuvunja mkataba huo wa mwaka 1898, vinginevyo hadi leo ungekuwepo. View attachment 1409011

@military_Genius
 
Back
Top Bottom