Nimefarijika sana kuona youtuber akifanya kazi nzuri kuitangaza Tanzania na miji yake kwa waTanzania na ulimwengu kwa ujumla.
Tulikuwa tunamsikia Regional Commssioner wa zamani wa mkoa wa Tabora mzee Aggrey Mwanri akituambia kupitia vyimbo vya habari uzuri wa mji wa Tabora na utunzwaji wa mazingira ya miundombinu na ukijani wa miti iliyopandwa.
Sasa tunapata bahati kupitia matumizi ya bora ya TEHAMA kuona kwa macho na kupitia uwakilishi mzuri wa mdau muonekano wa mji huu wa Tabora.
Mwanri alijitahidi sana kwenye utunzaji wa mazingira, ukiwa unaingia Tabora utaanza kukaribishwa na miti mizuri kando kando ya barabara achilia mbali ndani ya mji. Ni vyema mikoa mingine ikajifunze kwa Tabora.