Asante mkuu Kwa hili ila tutafakari kidogo, kwanini mwaka 2013 M23 walivyotandikwa wengi wao walikimbilia Rwanda na baadhi Uganda!?.
Baada ya miaka kadhaa kupita hili kundi lilikuja Kwa nguvu zaidi likiwa na vifaa vya kisasa, mbinu zaidi nk na huo moto wanauendeleza Hadi sasahv.
Lakini kama hili kundi ni threat Kwa serikali za Congo and Burundi we unadhani ni nani anayelifafhili!?
Hao wanaotwangana ni vivuli tu, huo mgogoro una chain ndefu, kuanzia hawa hawa wakongo, warwanda, waganda, waburundi, kenya na baadhi ya nchi za kiafrika ata Tanzania ikiwemo.
Back up kubwa wanaitoa kutoka nchi za Asia kama israel, Qatar, nchi za ulaya baadhi na USA kama main character asiyejulikana na wengi lkn ndie mnufaika wa the final product kutoka chain nzima ya mali kutoka kwa migodi iliyochimbwa kinyemela na mali kuuzwa kinyemela na hawa waasi/kinyume na sheria then zinawafikia ndugu zenu wa hapo rwanda wanazichakata zinakwenda hapo uarabuni baadhi ya nchi then hizoo ulaya+marekani kwa watumiaji wakuu (Tesla& Apple) ni mfano wa wanufaika wa mali za Congo, huyu tesla chini ya Elon ndie mnunuzi wa madini Yatumikayo kuunda mabetri ya magari ya umeme ya Tesla+cybertrucks, pia huyo Apple mnamjua mnunuzi wa madini kwaajili ya electronic devices.
Kiufupi huu mgogoro una wanufaika na acters wengi kuliko migogoro mingi hapa duniani, na niwajulishe hawa wapumbavu ambao wanasema Kongo haiingii hata top 5 ya nchi zenye rasilimami duniani, sijui akili zao bado wanategemea documents za mzungu kusema lipi ni lipi na lipi ni lipi? hivi hao Russia na nchi za uarabuni zingekuwa na rasilimali bado wangeendelea kuja hapa Afrika?😅.
Russia na baadhi ya nchi mnazosema zina resources nyingi walizozizidi Congo au nchi ya Tz ni wingi wa mafuta tu, lkn kwa Congo na baadhi ya nchi za kiafrika kuna resources nyingii na ambazo bado hazijagunduliwa, pia zipo zilizogunduliwa lakn bado matumizi yake hayajawekwa wazi, pia zipo ambazo zimegundulika ambazo ndizo hitaji kubwa hasa kwa FUTURE TECH ktk matumizi ya Semiconductors na technolojia ya nishati safi isiyoharibu mazingira.
Congo ina mengi ambayo hamuwezi kuyajua kirahisi mpaka mchimbe taarifa hasa kuzipata Kwa wacongo wenyewe au leaked infos kutoka ktk vyanzo mbalimbali.
Mgogoro wa Congo kuusolve kwake ni either waCongo wakubali kuachia ardhi yao imegwe na kugawanywa kwa baaadhi ya wacongo wasaliti wanaoshirikiana na nchi za kigeni, au au wacongo wenyewe waamue la kuamua kusolve tatzo wao wenyewe jambo ambalo ni gumu hasa kwa kizazi cha kipuuzi cha sasa.
Afrika bado iko utumwani ndiomaana bado mnaaminishwa eti kuna nchi nje ya Afrika inazizidi nchi za Afrika kwa wingi wa rasilimali, kumbe uzushi mtupu, hawa ngozi nyeupe kama waliweza kudanganya ukubwa wa Afrika na maajabu yake mnadhani wataweza kuwapa sifa zenu?