Mjinga mmoja wa IT ameniulia gari langu

Wewe umejuaje huyo ni mjinga wa IT?
 
Pole kwa majanga hayo. Je, bima ulikata tena kubwa au?!
 
Jitahidi kesi iende mahakamani , bima yake italipa
Mahakamani kesi inakaa muda gani, na kipindi hicho unatumia usafiri gani na wakili wako analipwa na nani? Na nani anai tow gari kutoka njia panda Dodoma kuipeleka garage karibu na unakoishi ili uweze kuifuatilia kama BIMA wataamua kui fix?

Ajali sio suala rahisi kama unavyomwambia eti arilaksi!

Police report yenyewe unaweza kuifuatulia mwezi mzima wanajidai polisi mhusika yuko msibani, wanataka rushwa.

Na gereji za Wachina nazo (supposed to be the best of all) usidhani wako profesheno kiviiiile, wanahitaji kuwafuatilia kama garage zetu za Kiswahili.
 
Nadhani huna uelewa na traffic cases
Gari hupeleki kwako.. Inavutwa kwenda police
Huhitaji wakili na ni kesi zinazoamuliwa haraka kuliko kesi nyingine zozote
Towing charges hulipi siku hiyo na mara nyingi bima ndio hubeba huo mzigo
Kinachotakiwa ni nyaraka zifuatazo toka police
PF 90... Hii ni ya kutoa taarifa ya ajali na ukaguzi wa polisi
PF 91 ... Mchoro wa ajali pamoja na maelezo ya dereva
PF 115 ... Hii ni ya hukumu
Vingine ambavyo si vya polisi
Cover note na receipt
Leseni
Claim form
Quotation
Nknk
Traffic case nyingi hazimalizi mwezi
Huyo kesi yake ni nyepesi kwakuwa kafuatwa upande wake
 
Hukumu inatolewa polisi ?
 
Kuna kesi haziendi mahakamani...zinaishia police ila kwa PF 115 inatolewa mahakamani..... Lakini utaichukua police kwa traffic mwenye kesi yako
kuna kesi haziendi mahakamani ? Wewe ndio umesema tuhakikishe kesi inaenda mahakamani. Sasa imekua tuyamalize polisi ?

Halafu PF maana yake ni Police Form. Mahakama inatoaje Police Form?

Na kwa nini niko mahakamani halafu hukumu ya kesi yangu apewe polisi ????

Halafu kwa Tanzania hapa hayo ma fomu 10 kidogo huwezi kuyapata na ku fixiwa gari lako au kulipwa ndani ya mwezi mmoja!

Na gharama za tow truck huwezi kuiita halafu umwambie vuta gari kisha utalipwa kesi ikiisha! Hesabu ya siku anaipelekaje? Na wewe uliyemuita ukishindwa kesi inakuaje ?

Ongea uhalisia brother.
 
Mkuu shukuru MUNGU sana kutoka salama kwenye ajari hiyo, hivi vyombo vinatafutwa tu......najua inauma mtu umejichanga umepata kausafiri...ila kwa hiyo ajari mshukuru sana MUNGU.......
 
Nimesema kuna kesi haziendi mahakamani sijasema hiyo
Kwenye PF 115 ndio kunaambatanishwa na nakala ya hukumu
Kesi zisizoenda mahakamani ni zile ajali binafsi na zisizo na majeruhi au kifo.. Yaani mtu kagonga jiwe au mti nk hakuna madhara au uharibifu wa vitu vya wengine

Breakdown hawapeleki hesabu ya siku wanapeleka kwa gari .. Na hii biashara wamiliki mara nyingi ni waajiriwa ndani ya Jeshi la polisi
Huwezi kukimbia na pesa yao kwakuwa gari na nyaraka zako vinakuwa mikononi mwao
 
Okay

kwa hiyo PF 115 siyo hukumu!

na hukumu ya kesi yangu niko mahakamani hapewi polisi , NAPEWA MIMI!

ulianza kwa kunichana kwamba sijui mambo ya BIMA na mahakama

tuendelee mdogo mdogo

Nani analipa tow truck siku ya ajali ??????
 
Okay

kwa hiyo PF 115 siyo hukumu!

ulianza kwa kunichana kwamba sijui mambo ya BIMA na ajali

tuendelee mdogo mdogo

Nani analipa tow truck siku ya ajali ????
Siku ya ajali huiti wewe breakdown zipo tu huko kwenye vituo vya polisi na maranyingi wanaoitisha ni madalali wao au traffic wenyewe
Siku hiyo huwezi kudaiwa hata senti moja
Hukupanga upate ajali
Pengine umepoteza pesa, simu na card ya bank
Pengine umejeruhiwa na kuumia vibaya
Pengine umekufa
Si gari zote zinazopata ajali ziko na wamiliki wake, wengine ni ndugu ama ni madereva
Kwahiyo breakdown ana kazi ya kuondoa gari sehemu ya ajali na kuipeleka polisi na ana jukumu pia la kuilinda isiibiwe chochote
Vilevile si ajali zote tunapata tukiwa maeneo yetu

Siku utakapoanza kufuatilia polisi ndio utapewa gharama na kama bado huna hawana haraka pia
 
Okay sawa

Yule dereva wa break down naomba kujua siku ya ajali analipwa na nani, polisi au anaitwa halafu halipwi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…