Mjini kuwe na affordable English courses tunaadhirika

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ni huyu shost alikutana na kijana wa ki Tanzania anaeishi ughaibuni kwenye harusi, kijana akiwa hajaoa alimchumbia shost sasa baada ya harusi shost anakwenda ughaibuni kama spouse.

Jamani afadhali wa Masaki na Mbezi wanatupia vile vineno "you know that is not acceptable ", Huyu shost ni wa kwetu Kwamtogole, habari ya huku ni "mama Irene unikome".

Safari ya shost ilikuwa ya masaa nane kwenye ndege, check in ilikuwa saa tano na ndege iliondoka saa saba mchana. Bibi yule tangia chai aliyokunywa kwao asubuhi mpaka anaingia ughaibuni hakula kitu chochote. Kila kilichopitishwa kwenye ndege alisema "no thank you" akiogopa majibizano ya zaidi, pia alihifia masikini kama chakula kinauzwa hayo majibizano ya bei yatakuwaje?
 
Alisahau kubeba ile kamusi ya Swahili-english ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Ras simba na zile formula zake za sijui nini plus nini anchaji kiasi gani, maana anakwambia ndani ya mwezi kama hujajua kiingereza basi labda ukazaliwe UK
 
Kwani Ras simba na zile formula zake za sijui nini plus nini anchaji kiasi gani, maana anakwambia ndani ya mwezi kama hujajua kiingereza basi labda ukazaliwe UK
Bei ya RAS Simba iko juu kwetu sisi wapika maandazi na chapati na kumbe zali la kupanda ndege lunamuangukia yeyote yule.
 
Ni Ujuha tu Kwa Watanzania kushindwa kujua ata basic za English ivi hizi smartphone zetu, Tablet tunazitumia Kuperuzi picha za celebrities wa insta, Leo huhitaji kabiss mwalimu wa kingereza simu yako ni mwalimu tosha kama una nia ya kujifunza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hiyo lugha ngumu jamani mtu akianza kuongea hata kama nakula njaa inaanza kuuma tena
Hahah Kikiristo sio lugha ya kispot spot bora uyo kakubadili Kupanda Ndege mwenzie ataki kusikia Inshu za Pipa kabisa na u Dr wake
 
mama irene unikome.
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Wanasema ushamba mzigo...Huyo shosti wako hakuwa na nia ya kujifunza English course tu
 
Kuna jamaa yangu kaoa mchina, Mkewe yupo bize kila mda anachat kwa yale maandishi ya karate, jama naye yupo bize na maandishi yetu ya profesa Lipumba... Kweli jazwa Ujazwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…