Acha umbea wewe...Hutu jirani yangu aliyekuwa analalamika vyuma vimekaza leo anawacheka wanaolia na hali ngumu. Kumbe mpwa wake anaefanya kazi kwenye taasisi nyeti amempigia pande la kumfundisha mapishi mtoto wa kigogo.
Mwanafunzi anakuja Jumamosi na kapu la mazagazaga. Shost akisema ni darasa la chapati basi mwanafunzi anatumwa unga kilo 5. Mafuta litre mbili
Mjini shule jamani, Dar form six