Mjomba Twalib. Unayofanyia wenzio Mola anakuona. Akhera utajibu nini Sheikh wangu?

Gobole Lenye Risasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
11,519
Reaction score
23,693
Naandika kwa hasira na uchungu. Sikutaka niandike lakini nimeona niandike sababu najua mhusika hayumo humu. Ila hata akijaambiwa wacha ajue itasaidia maana sijaweza na sitoweza mwambia usoni.

Wiki iliyopita Mjomba alituita kwake Mbagala kwa Mke mdogo. Ilikuwa ijumaa alituambia kulikuwa na kisoml alimwita Sheikh akamsomee. Alichinja Mbuzi mmoja mkubwa mweusi. Mimi nlienda sababu nliitikia wito na huwa wanasema mara nyingi sijichanganyi nao sababu nina ukafir kafir mwingi.

Likipigwa na biriani tulikuwa watu kama 20 hivi. Mimi sikula ile nyama. Nina utaratibu wangu tu wa kijinga huwa sili vitu vya kafara. Actually ni mzee alinidokeza hilo pia miaka ya nyuma maana ilikuwa ni jambo la kawaida kufanya hivyo tukiwa tunaishi Tandika.

Baadaye Mjomba Twalib alikuwa akiongea na Sheikh ( sitomtaja jina) aliyemsomea kisomo. Kuwa majibu yatapatikana ndani ya siku 7. Wala asiwe na wasi.

Leo Mjomba kanipigia akiwa na furaha sana ananiuliza namkumbuka yule sheikh wa siku ile? Nikamwambia ndiyo. Anasema yule sasa ndo sheikh siyo wengine wababaifu. Nikiwa na shida nimjulishe. Ametengeneza kitu watu wameanza kutoa milio.

Mjomba wangu ni wa miaka 57 au 58.alisoma mpaka kidato cha nne tu. Akawa anafanya kazi kama dereva shirika moja la mafao. Baadaye akapandishwa cheo akiwa anaonekana ana diploma ya mambo flani ambayo aliipata Chuo flani. Mi namjua Mjomba hana hiyo elimu. Yaani ni mweupe tu.

Kipindi kile cha vyeti fake kuna namna alifanikiwa kutofutwa kazi. Yeye alitamba kuwa alisafiri Tanga kuhakikisha hilo halitokei. Akabaki. Amependa panda tuvyeo na diploma yake kwa namna ambayo hatuwezi elezea. Tunashukuru ni mjomba wetu.

Sasa kazini wamekuja vijana wana elimu na uwezo wa ukweli. Inasemekana kuna kijana alikuwa anaonekana kupendekezwa kuchukua nafasi ya mjomba maana mjomba anaonekana tu kiuhalisia nafasi yake ni ya kubebwa bebwa sana uwezo hamna. Hizo tetesi kazipata.

Ndo kumwita mtu wa kisomo. Kimefanyika ijumaa iliyopita. Huyo kijana leo kafika ofisini kateleza kaanguka vibaya na mguu umevunjika pamoja na mkono. Kwa maelezo ya mjomba kijana atalala sana nyumbani na safari ambayo ilikuwa aende kwenye mafunzo ya wiki 2 nje ya nchi sasa ataenda yeye Mjomba Twalib.

Nimewaza sana. Hawa wazee wa aina ya Mjomba Twalib ni wengi na wanaharibu nguvu kazi ya vijana kwa roho zao mbaya. Imeniumiza sana why binadamu tuwe wakatili namna hii. Yeye anaongea kwa kujigamba sana kuwa sasa watamjua yeye ni nani maana walianza mzoea. Kwa maelezo yake huyo kijana katupiwa jini ahangaike nalo.

Nawaza najiuliza na namuuliza Mjomba Twalib. Ukienda Akhera utasema nini? Je ni sawa mbele za Mola wako? Nawe ni mtu wa swala sana Mjomba.
 
images (1).jpeg
 
Mjomba wenu lazima ni kada kindakindaki wa CCM
 
Ndefu sana naomba samari
Mjomba Twalib kamvunja mguu mfanyakazi mwenzake kazini kwa kafara la mbuzi mkubwa mweusi...
Aliyevunjika atakua kitandani anajiuguza kwa muda mrefu sana, sababu jamaa aliletwa kuchukua nafasi ya mjomba twalib...
 
Dahhhhh!!! Inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom