Mjomba wangu anataka kuchomwa akifa, familia yake imekataa kaja kwangu, Nichukue uamuzi upi??

Mjomba wangu anataka kuchomwa akifa, familia yake imekataa kaja kwangu, Nichukue uamuzi upi??

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264

Kwa kipindi kama cha miaka mitatu amekuwa akiwa na msimamo wa kutaka kufanyiwa mazshi kwa kuchomwa mauti yakimkuta

Sababu zake mpaka sasa hazijaniingia akilini, yeye hataki mwili wake uoze taratibu, sijui mambo ya mwili kutumika msukule, kuhofia kwamba ataamka akizikwa 😂 😂 n.k.

Familia yake ilikataa kwa hio kaja kwangu, kaniomba nimsaidie hio ishu na pia niende kupeperusha majivu yake kijijini sehemu aliyokuwa akiipenda utotoni.

Huduma hii ya mazishi natambua kwamba ipo hata hapa nchini, inaitwa cremation, lakini imezoeleka kwa kiasi kikubwa kutumika na wahindi wanaofata mila na tamaduni zao.

Kwa tamaduni zetu hizi za hapa kwetu na hata kwa dini, huu utaratibu haujazoeleka kiukweli, kwa hiyo hata mimi siwezi kumtekelezea anachotaka, pia hata familia yake nayo imekataa, sipendi kuanzisha taharuki.

Huwa nampaga tu sapoti ya kinafki 😁 maana ni mjomba tuliezoeana sana.

Je nimwambie ukweli kwamba sitaweza kutekeleza anachotaka au nimdanganye tu ili kumfurahisha ila kama kawaida maafa yakimkuta atazikwa tu kwa utaratibu wa kawaida.
 
Ni uncle wangu yupo kwenye 50 huko.

Kwa kipindi kama cha miaka mitatu amekuwa akiwa na msimamo wa kutaka kuchomwa akifa.

Familia yake ilikataa lwa hio kaja kwangu.

nami sio muumini wa hizi ishu.

Je nimwambie ukweli sitaweza kutekeleza anachotaka au nimfanganye tu ili kumfurahisha, ila kama kawaida maafa yakimkuta atazikwa tu.
Anayetaka kuchomwa ni yeye, sasa mnamkatalia vipi?
 
pagumu mkuu.

ila nchi za wenzetu huo ni uamuzi wa mtu binafsi, na wengine wanagawa kabisa viungo vyao kwa ajili ya research za spitali au kuwasaidia watu wengine.
Naomba Sana kila siku nilitaka kufa mungu anipe kauli ya mwisho ambapo nataka moyo,Figo na maini yangu vivunwe na kuwasaidia watu ambao wanavyo uhitaji.

Ile sheria ya uvunaji wa viungo naisubiri kwa hamu sana
 
Anataka achomwe moto akifariki. Hataki kuwa mzimu?
 
Naomba Sana kila siku nilitaka kufa mungu anipe kauli ya mwisho ambapo nataka moyo,Figo na maini yangu vivunwe na kuwasaidia watu ambao wanavyo uhitaji.

Ile sheria ya uvunaji wa viungo naisubiri kwa hamu sana
Mkuu Bora uzikwe na viungo vyako tu.
 
Naomba Sana kila siku nilitaka kufa mungu anipe kauli ya mwisho ambapo nataka moyo,Figo na maini yangu vivunwe na kuwasaidia watu ambao wanavyo uhitaji.

Ile sheria ya uvunaji wa viungo naisubiri kwa hamu sana
Siku ya ufufuo utaulizwa figo uligawa kwa nani? Halafu utabaki unambwelambwela hapo ndio utaelewa Tanzanite kwao Tanzania
 
Mwenyewe nimeomba nizikwe mahali nitakapoishi daima sitaki mwili wangu kuzungushwazungushwa.MTEKELEZEENI
 
Mwambie asijichoshe,Tanzania hatuna utamaduni huo,japo yeye anaupenda kwa hiari yake!!

Mchane ukweli, ukimdanganya halafu akafa usimfanyie hivyo,nafsi inaweza kuwa inakusuta na hali hiyo itakutesa sana!
 
Mwambie ukweli kuwa huwezi ukimdaganya akifa na asichomwe mzimu wake utakutesa mpaka ufanyiwe matambiko ya kimila shauri yako
 
Back
Top Bottom