SoC04 Mjongeo wezeshi

SoC04 Mjongeo wezeshi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Naomi Fumbuka

New Member
Joined
May 16, 2024
Posts
1
Reaction score
1
"Ukiona vyaelea jua vimeundwa "TANZANIA TUITAKAYO” ndani ya miaka mitano Hadi ishirini na tano ijayo, utekelezwaji wa matumizi sahihi ya Rasilimali asili kama vile aridhi ambayo ndiyo utajiri muhimu, ikumbukwe kuwa takribani ya kilometa za mraba 947,303 inayopatikana nchini Tanzania imekusanya urithi wa madini mfano dhahabu,makaa ya mawe,Tanzanite,pia misitu ya asili,vyanzo vya maji, watu na wanyama.

Ambayo huleta mchango wa maendeleo nchini kwa kujipatia fedha kutokea kwenye uwekezaji wa viwanda, utalii wa ndani na wa nje kitendo ambacho kinapelekea ongezeko la kipato Cha thamani ya fedha ya Tanzania. Hivyo uboreshwaji wa uwekezaji itapelekea nchi kuwa na uchumi Bora na imara zaidi

Kwa mantinki hiyo, Rasilimali asili ziweze kuishi miaka mingi na kuleta matunda inatakiwa serikali iwashirikishe wananchi katika mfumo mzima wa hifadhi na matumizi ili kuwapa kipaumbele wananchi katika maswala yote yanayohusu Rasilimali asili na hiii utafanya wananchi kuweka ulinzi na sio kujali masilahi ya wawekezaji pekee.

Mfano,Rasilimali za misitu ni Mojawapo ya vivutio vya utalii, ni sehemu ya ongezeko la mkusanyiko wa mapato katika serikali, ili kuweka wajibu wa kulinda Rasilimali hizi sera kali ya ukataji miti ovyo bila kuchukua juhudi za upandaji miche mipya litiliwe mkazo kwani kuendelea Kwa nwenendo huu utafanya kupoteza aridhi yenye rutuba ambayo itapelekea umasikini na majanga ya njaa hatimae kuwa ombaomba na wingi wa madeni kutoka mataifa mengine

Vilevile kutekelezwa Kwa ongezeko la uboreshwaji wa miundombinu mfano Barabara za nyanja zote zitakazotumika kusafirisha wazawa kutokea sehemu Moja kwenda sehemu nyingine Kwa ajili ya shughuli za Kila siku katika utafutaji ridhiki,wageni kutokea nchi mbalimbali ili kuifikia Tanzania katika utalii, uzalishaji wa bidhaa kutoka viwandani hutegemea miundombinu Bora ili bidhaa hizo zifike mahali palipokusudiwa na kadiri miaka inavyozidi kusogea ndipo tekinologia inaongezeka uboreshwaji wa miundombinu itasaidi kilimo kuimalika Kwa kuwa ndio uti wa mgongo wa Tanzania, na ubunifu wa kiuchukuzi uongezeke Tena na Tena.

Sera ya uchumi imara Kwa vitendo Tanzania,Kwa kiasi kikubwa hapa nchini wananchi wamejikita katika mgawanyiko wa shughuli za kiuchumi mfano kilimo,ufuguji,ujasiliamali na uchimbaji wa madini, kama kwenye shughuli hizo zikipewa kipaumbele Kwa upande wa kilimo Kwa kutoa misaada ya pembejeo,maeneo na umwagiliaji bila kutegemea misimu ya mvua itapelekea uvunaji wa mazao mengi Kwa zaidi ya misimu mitatu Kwa mwaka, Sasa chakuzingatia maeneo ya vijijini walau Kwa Kila Kijiji kipokee jeneleta za umwagiliaji ili iwe tija ya ongezeko la mazao ya chakula na ya kibiashara yawepo Kwa wingi, utoaji wa mikopo na elimu kwa wajasiliamali na wafanya biashara wakubwa, pia vifaa stahiki vya uchimbaji wa madini ili kupunguza upoteaji wa nguvu ya taifa ususani vijana Kwa kukubwa na matokeo ya hatari ya maeneo hayo bila kuharibu mazingira na vyanzo vya maji.

Hili pia lizingatiwe usawa wa huduma za kijamii mjini na vijijini, sehemu kubwa maeneo ya mjini Kasi ya huduma za kijamii zipo na zizidi kuwepo lakini isiwe ya kasi Sana ili vijijini ipewe nafasi ya kupata umeme wakutosha,maji Safi na salama,vituo vya afya, na vituo vya polisi,ndani ya miaka ijayo itasaidia kupunguza mjazano wa watu katika eneo Moja kwani wananchi watahamia vijijini hii itapunguza wa magonjwa ya mlipuko hasa yanayoambukizwa Kwa njia ya hewa

Elimu Bora na yenye kujitambua Tanzania,mpangilio wa elimu Bora pekee ya kuongeza wataalamu wa kutosha na majengo mazuri haitosaidia Kwa mtanzania, Bali ni yenye kujitambua na kutumia mtaji wa akili aliyonayo Kwa maana ya kwamba mwanafumzi wa shule ya msingi,sekondari,chuo anapokuwa shuleni apate ufahamu wa kuwa baada ya masomo kunamaisha asikae kuelewa mtaala wa masomo shuleni Ila apate kuondoka na uwelewa utakao msaidia kukabiliana na maisha, hii ni vema kama wazazi, walezi na serikali Kwa ujumla kuzingatia vipaji vya wanafunzi kama vile uchezaji wa mpira nyanja zote,usanii,ubunifu na uongozi wa kiutawala ili alichojifunza darasani kikalete matokeo katika maisha yake hii itasaidi kuondo idadi ya kupotelewa na nguvu kazi ya taifa mfano vijana kujiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya hata kujiua Kwa msongo wa mawazo, watu tegemezi na wahalifu.

Mpango wa ajira ujikite katika mshahara na kazi,utaratibu wa waajiriwa kusubili mshahara mwisho wa mwezi huongeza uvivu hasa maofiaini, kwani kujituma hupungua na badala yake linabaki suala la kuangalia namna ya kukabiliana na njaa ndio sababu njia za Chocho hutumika kama upokeaji na utoaji wa rushwa ya pesa na ngono, kufanyiana mipango ya ndugu na ndugu kuingia kazini bila kigezo sahihi. kama mtu atapewa ujira wake unaositahili maendeleo yataongezeka mfano mfanyakazi anapoingia ofisini na kukaa tu bila kujituma nakusubili muda wa kurudi nyumbani alipwe hata shilingi 2000 hata kama analipwa Kwa mwezi laki 4.

Tanzania tuitakayo ni siasa ya maendeleo na sera ya uongozi Bora,licha ya kwamba maendeleo yote kuhusu wananchi yanaamuliwa na siasa ni sahihi kwamba mtu hujifunza kupitia makosa na sio kuwa na chuki, Kwa sababu Tanzania ni ya kidemokrasia ni vema chama kimoja kikosoe kingine Kwa ajili ya kurekebishana na kuleta maendeleo na si tu kufanya maandamano, viongozi wa kisiasa wajikite katika kufanya wajibu wao.

Mara zote husemwa mcheza kwako hutunzwa mkataa kwao mtumwa,uthaminishwaji wa uwepo wa urithishaji wa utamaduni chanya kutoka kwenye makabila kama Moja ya kulinda kupotelewa Kwa lugha za asili na ikumbukwe kuwa Tanzania ilipata mafanikio katika upande wa kujenga hisia za utaifa baada ya kufanikiwa kufanya makabila yaliyokuwa yakizungumza lugha za asili kuunda lugha Moja ya kiswahili Vilevile ulaji wa vyakula vya asili ili kuimalisha mili na kuepukana na magonjwa kama vile saratani.

Mbali na mtaji wa mtu ni akili pia afya inahusika, serikali ifanye jitihada za kuwapeleka wasomi wa maswala ya afya baadhi ya nchi bobezi Kwa ajili ya kupata mafunzo na kuongeza utaalamu zaidi, na kuongeza vifaa tiba pamoja na kutoa elimu ya afya Kwa wananchi kupitia vyombo vya habari, semina, makongamano, matamasha, mikutano na mikusanyiko mfano namna gani ya kuepukana na magonjwa ya kuambukiza na yasio ya kuambukiza, ili kupunguza vifo vya wagonjwa wasio na uwezo wa kusafiri kutoka nchi Moja kwenda nchi nyingine Kwa ajili ya matibabu, hii itasaidia Sana kupunguza misaada Kwa wahitaji na badala yake kuleta maendeleo Hitimisho"Tulinde tulivyonavyo na kuvithamni Tanzania kwani aliyenacho huonezewa" Na.NAOMI FUMBUKA (madame msimbo).
 
Upvote 4
Hili pia lizingatiwe usawa wa huduma za kijamii mjini na vijijini, sehemu kubwa maeneo ya mjini Kasi ya huduma za kijamii zipo na zizidi kuwepo lakini isiwe ya kasi Sana ili vijijini ipewe nafasi ya kupata umeme wakutosha,maji Safi na salama,vituo vya afya, na vituo vya polisi,ndani ya miaka ijayo itasaidia kupunguza mjazano wa watu katika eneo Moja kwani wananchi watahamia vijijini hii itapunguza wa magonjwa ya mlipuko hasa yanayoa
Safi kabisa, vijiji viwe vya kisasa na vya kuvutia watu tukaishi huko.

i. kama mtu atapewa ujira wake unaositahili maendeleo yataongezeka mfano mfanyakazi anapoingia ofisini na kukaa tu bila kujituma nakusubili muda wa kurudi nyumbani alipwe hata shilingi 2000 hata kama analipwa Kwa mwezi laki 4.
Hapa sijaelewa: kwamba unataka watu walipwe hata kama hawajafanya kazi au. Na mtu anapolipwa baada ya kufanya kazi haya malipo mengine ni kwa ajili ya nn dada?

Tanzania ilipata mafanikio katika upande wa kujenga hisia za utaifa baada ya kufanikiwa kufanya makabila yaliyokuwa yakizungumza lugha za asili kuunda lugha Moja ya kiswahili
Nyerere alicheza vema sana asee.
 
Back
Top Bottom