I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
BEAVERS ni jamii ya panya na niya pili kwa ukubwa kati ya jamii za panya wote waishio kwa sasa. Wanapatikana sana Katika ukanda wa kaskazini kama Amerika ya kaskazini na ulaya ya magharibi.
Kimaumbile wana urefu wa kuanzia mita 0.3 hadi 0.5 (kuanzia kichwa hadi mkia), na kiupanna sentimita 30-60. Kwa maumbile ya miili jinsia zote mbili hazitofautiani ukubwa.
Ni wanyama wanaoishi kando kando na vyanzo vya maji baridi mfano mito, mabwawa na hata madimbwi. Wanyama hawa wamejaliwa uwezo mkubwa wa kupiga mbizi ndani ya maji au muda mwingine na pengine hupendelea sana kuelea tu juu ya maji; njia hii huwasaidia sana hasa katika kujilinda na maadui zao kama mbwa mwitu na mbweha
Hawa jamaa ni wataalamu sana katika maswala mazima ya ujenzi. Hutumia taaluma zao kujenga viota ndani pembezoni ya maji kwa kutumia nyenzo mbalimbali kama matawi ya miti, vipande vya magome ya miti, mimea tofauti tofauti, mawe na udongo kwa pamoja. Hivi vitu vyote humpa uhakikisho kuwa makazi yao yapo salama na hayapitishi maji kuingia ndani. Pongezi nyingi kwa taya zao zenye nguvu sana kuweza kuangusha mti mkubwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Kihistoria, hawa wanyama wamekuwa wakiwindwa sana kutokana na ngozi zao, nyama na {castoreum (ni tezi mbili zinazopatikana katikati ya nyonga za beavers na mikia yao)}.
Hizi castoreum zilikuwa zikitumika kutengenezea madawa, perfum, na viongeza ladha kwenye chakula.
Mapema katika karne ya 20, uwindaji huu haramu ulipigwa marufuku kwa sababu ilibaki kidogo sana jamii hii ipotee katika uso wa dunia.