HELLEN JOHNSON SIRLEAF. ALIONDOKA IKULU BILA MIKONO YENYE DAMU.
-----------------------------------------------------
Hakuna damu iliyomwagika. Naondoka ikulu ya "Monrovia" nikiwa na mikono safi. Kama nitahukumiwa siku moja ni kwa dhambi nyingine. Lakini si ya kupora maamuzi ya uma kwenye sanduku la kura.
Hatuangalii nani ameshinda, tunaangalia nani atahakikisha nchi yetu ipo salama. Kiongozi mwenye nia na dhamira ya kutotaka kuturudisha kwenye makovu yaliyopita. Ndiye uma umemchagua. Hongera George Opong weah."
Hiyo ilikuwa sehemu ya hotuba toka kwa bi "Hellen Johnson Sirleaf." Tarehe 13 October 2017. Wakati anamuachia ikulu "George Opong Weah.
Bi Hellen Johnson Sirleaf. Ndiye Rais wa kwanza mwanamke katika bara la Africa kuingia madarakani kwa mfumo wa demokrasia. Alikuwa Rais wa 24 wa Liberia. Aliishi ikulu ya Monrovia kutoka mwaka 2006 - 2018.
Wakati anamkabidhi George Weah ikulu. Weah alikuwa mgombea kutoka chama cha upinzani.
Mgombea wa chama chake aliyekuwa makamu wake wa Rais. Alishindwa katika marudio ya uchaguzi.
Bi Hellen alikuwa na uwezo wakutumia jeshi kulazimisha mrithi wa kiti cha u Rais atoke chama chake.
Lakini hakuanguka kwenye shimo la upotofu. Sababu miwani ya macho ilimsaidia kusoma alama za nyakati. Hakutaka kuirudisha Liberia jekhanam ya damu.
Hili lilikuwa darasa la ukomavu wa demokrasia. Na somo la vitendo, jinsi ya kukabidhi ikulu bila kuacha alama ya maafa."
Mabaki ya mafuvu, makaburi ya halaiki, video za watu waliopata ulemavu, na tabaka kubwa la waliopoteza makazi sababu ya vita. Ni taswira iliyoyachukiza macho ya Bi Hellen.
Enzi za uongozi wake aliiunganisha Liberia. Aliua ukabila na itikadi za ki siasa. Alilileta taifa pamoja. Mifumo kandamizi akaichimbia kaburi.
Aliponya majeraha kwa kauli za hekima. Vikao vya umoja wa kitaifa vilifanyika mara kwa mara. Kila kinywa chake kilipofunguka, alihakikisha neno "Amani" limehubiriwa.
Hakuruhusu matajiri kuzinunua sheria. Wala hakutaka rimoti za mahakama ziishi ikulu. Aliacha mihimili ijiendeshe kwa kufuata misingi ya sheria usawa na haki.
Liberia iliyokuwa imeoza mifumo. Nchi yenye harufu ya uvundo wa damu. Watu wakichinjana sababu ya kutofautiana mitazamo hoja na itikadi. Hatimaye ilianza kubadilika.
Ikawa nchi ya maziwa na asali. Kinywa kilichozoea damu kikaanza kufurahia matunda ya amani. Ujio wa bi "HELLEN SIRLEAF" ikulu ya Monrovia. Ulileta ukombozi wa kiroho.
Hili lilikuwa somo kubwa. Funzo la vitendo juu ya utawala bora toka kwa Rais mwanamke.,"
Ulimwengu uliyaona matendo mema ya Hellen sirleaf. Juhudi za kuiunganisha Liberia zilimlipa heshima. Mwaka 2011 dunia ilimzawadia tuzo ya "NOBEL."
Katika moja ya interview bi Hellen Sirleaf aliwahi kuulizwa swali hili. Je! ni kwanini nchi nyingi za Africa maandamano yanakithiri?!
Hivi ndivyo alivyojibu:
"Uroho wa madaraka na uzito wa kusoma alama za nyakati. Hili ni somo linalowafelisha wanasiasa wengi kwenye mtihani wa kulinda amani."
Hili halikuwa jibu la kawaida. Bali sauti ya ki Mungu kwenye kinywa cha mwanamke. Ambaye hekima imechagua kuishi ndani ya ubongo wake."