Mjue binadamu wa ajabu anaitwa Unju bin Unuk

Mjue binadamu wa ajabu anaitwa Unju bin Unuk

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Hivi ushawai sikia story za mtu kiumbe kiitwacho Unju bin Unuk?

Basi ngoja nikusimulie kwa ufupi!

Unju bin Unuk ni mtu aliepata kuishi zamani inakadiriwa aliishi karne ya 16-17 uyu jamaa kuna watu wanamsema ni moja ya manabii, wengine wanasema ni mtu tu wa maajabu.

Unju bin unuk alikuwa na urefu mkubwa sana na mwili mkubwa kuwahi kutokea duniani alikuwa ana uwezo wa kuingia baharini na akaokota samaki kwa mkono akiwa ndani ya maji na akamkausha na jua kwa kunyoosha mkono juu na kurikalibia jua.

Pia jamaa inasemekana alikuwa na uwezo wa kutembea kwa kuruka ruka; jamaa inasemekana hata Tanzania alishawai kuwepo alipata kuishi maeneo ya Kilwa Kivinje na kaburi lake ndo Lipo uko.

Jamaa inasemekana hatua yake moja ya mguu wa kulia ipo Tabora na nyingine ya mguu wa kushoto ipo Kongo.

Pia inasemekana aliwahi pita maeneo fulani ya Kilwa akakuta watu wanachota maji mtoni akawaomba maji wale watu wakamfukuza ila tangu walipomfukuza yale maji ya ule mto yakawa machungu na yanawasha ila maji yale yale ya ule mto katika kijiji cha pili ni mazuri tu yanafaa kwa matumizi.

Je, vipi na wewe ushawai sikia habari za uyu mtu Unju bin Unuk.
 
Je Unju Bin Unuk ana connection na Uj Bin Anak?
 
Je Unju Bin Unuk ana connection na Uj Bin Anak?
Munasaba wake ni huyo huyo,ila habari hizi hazina ushahidi bali ni katika visa au habari za Waisraeli.

Aliitwa Uuj bin 'Anaq au Uuji bin 'Auq. Wanasema alikuwa Mfalme wa Bashaani na alikuwa kabla ya nabii Musa.
 
Mguu mmoja uko Tanzania ..halafu mguu mwingine uko Congo halafu maji ya kunywa aombe?Badala ya kuchota Kwenye mto Congo au mito yeyote ile?
Halafu apite kijijini Kilwa watu wafukuze?Huku huyo mtu ni mkubwa mguu mmoja uko Congo?
Baada ya kujiuliza mazwali kama hayo ndio maana me nimehitimisha tu kusema hii ni hadithi ya kusadikika kama zilivyo hadithi nyingine.
 
Munaba wake huyo huyo,ila habari hizi hazina ushahidi bali ni katika visa au habari za Waisraeli.

Aliitwa Uuj bin 'Anaq au Uuji bin 'Auq. Wanasema alikuwa Mfalme wa Bashaani na alikuwa kabla ya nabii Musa.
Kuna uwezekano hyu kiumbe aliwahi kuwepo duniani maana karibu kila bara wanamzungumzia kwa majina hayo ya Uj,Og,Unju,Oj n.k na sifa zake (Ingawa zinakuzwa) kama alizotaja mtoa mada ndio zinarudiwa kila mara story yake ikitajwa. Ssa imagine dunia ya kale hakuna simu wala mtandao kma sasa unao link taarifa za real-time.

Naweza fananisha na story ya Nuhu/Hud ambaye katika kila jamii mpaka umasaini wana amini huko nyuma kuna gharika lilitekrteza eneo lao na Njemba mmoja tu na famioia yake wakapona!! So unaweza ona story ikirudiwa sana randomly inaweza kuwa na ukweli sababu hawawezi wote kutunga kitu systematically over generations of varying nature.
 
Hizi ngano za kufikirika huwa nawasikia wahubiri wa dini fulani wakinukuu hadithi zao viroja kama hivi na waamini nao wanakubali na kushangilia
 
Back
Top Bottom