Mjue binadamu wa ajabu anaitwa Unju bin Unuk


Soma hiyoooo
 
Hadithi ni hadithi ndomana tunasema uongo njoo, ukweli njoo, utamu kolea. Nami natengeneza yangu muda sio mrefu [emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji28][emoji38]
 
Hii sidhani kama ni hoja sababu kitangaa kwa habari huwa inatangaa sana. Watu wakivutiwa na habari hupenda kuiweka katika lugha yao. Mfani mzuri visa vya Abuu Nuwas na mfano wa hivi,utavikut katika lugha tofauti na sehemu tofauti.
Lakini ukiangali habari za maumbile wa binadamu wa kale kwa wasifu tunao usikia kuhusu Unju bin Unuq,hakuna kiumbe kabla ya Musa alikuwa na umbile kama hilo.

Ili ujue kwamba hizi habari huenda kwa kurithishana,ungewauliza Wamasai hiyo habari waliipataje. Utaona ni kusimuliwa na watu fulani kisha habari ikawekwa katika lugha fulani.
 
hakuna kiumbe kabla ya Musa alikuwa na umbile kama hilo
Kwa reference ipi? maana wayahudi wenyewe kupitia vitabu vyao vya dini vinamtambua hyu OG na ambaye kwao ni mrefu kuliko yeyote kwenye Tanakh/Talmud.

Wakristo nao wanamtambua OG na vipimo vyake ni virefu kuliko umbo la Musa. Hata Rafa, Sihon, Anaki n.k hao wote ni warefu kuliko

Kwenye Qur'an... Surat Hud tunaona naye alikua Giant kweli kweli na hyu aliishi kabla ya Musa.

So tunaweza conclude kwamba kulikua na watu warefu sana kabla hta ya Mussa. And unless dini zimepotosha maana dini ZOTE zinaongelea pia hawa watu
 
Imebidi niende mtandaoni hadi Wikipedia na haya ndiyo niliyoyakuta nimecheka sana kwa kweli 😅 mlioko Bagamoyo mtuambie kama mmeona kaburi la kilomita 1 huko.

👇👇👇👇👇

Unju bin Unuq (pia: Unju bin Unuku, Unzi Bin Ununuk) ni jina la jitu katika masimulizi ya wakazi wa pwani ya Tanzania. Hadithi zake zasimuliwa kuanzia Bagamoyo hadi Kilwa.


Unju bin Unuq akibeba mlima anaotaka kuurusha dhidi ya Musa; picha katika nakala ya Kituruki ya Kitabu ‘Ajā’ib al-makhlūqāt (maajabu ya viumbe) كتاب عجائب المخلوقات وغرائب الموجودات cha Zakarīyā’ ibn Muḥammad al-Qazwīnī.
Historia yake inapatikana katika makumbusho ya Kaole huko Bagamoyo.

Moja ya mambo ya ajabu ya mtu huyu ni urefu wake yaani kimo, inasadikiwa alikuwa na urefu mkubwa ulioweza kumfanya atembee baharini na miguu yake kugusa chini.

Pia alikuwa akitembea kutoka nchi hadi nchi kutokana na urefu wake. Inasimuliwa kuwa mmoja kati ya nyayo zake unapatikana kwenye jiwe alilokanyaga huko Tabora, Tanzania, wayo wa mguu wa kushoto wakati wayo wa mguu wa kulia ulionekana kwenye jiwe alilokanyaga huko Kongo.

Inasimuliwa pia akitaka kula alikuwa akichukua samaki baharini kwa mkono na kuchoma katika jua kisha anakula.

Kuhusu maisha yake inasimuliwa kuwa Unju bin Unuk hakuoa wala kuolewa kutokana na umbo lake.

Sehemu nyingine ya hadithi yake ni alipokufa Unju bin Unuq, aligawanyika vipandevipande kutokana na urefu wake na inasemekana kidole chake chenye urefu wa kilometa moja kasoro ndicho kilichopatikana na kuzikwa pale Bagamoyo, lakini hakuna simulizi mwili wake uliobaki uliangukia wapi.

Unju bin Unuq alikuwa na ndugu yake aliyejulikana kama Geofrey bin Unuk, huyu alipatikana maeneo ya Dodoma. Au kwamba Unuq baada ya kupotea kwa muda wa miaka mingi ndugu zake wa mbali sana wameonekana katika mkoa wa Dodoma

Source: Wikipedia
 
Kwa reference ipi? maana wayahudi wenyewe kupitia vitabu vyao vya dini vinamtambua hyu OG na ambaye kwao ni mrefu kuliko yeyote kwenye Tanakh/Talmud.
Kwa marejeo ya Qur'aan na Hadithi za Mtume na Historia sahihi iliyo hakikiwa.
Kwenye Qur'an... Surat Hud tunaona naye alikua Giant kweli kweli na hyu aliishi kabla ya Musa.
Surat Hud aya ya ngapi tukasome kisha kisha turudi kwanye Tafsiri za Wanazuoni.
So tunaweza conclude kwamba kulikua na watu warefu sana kabla hta ya Mussa. And unless dini zimepotosha maana dini ZOTE zinaongelea pia hawa watu
Umewahi kuzihakiki hizi habari ?
 
Mtu wa kwanza kumtaja Unju mbele yangu alikuwa ni mama yangu, siikumbuki habari yote lakini nakumbuka kipengele cha urefu wa Unju
 
Hizi stori ndiyo za wakina mwana malundi
 
Too Much Tangawizi, Chai hainyweki kabisaaa.[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Na kaburi lipo kulwa... Itakua walimkataka kuanzia tabora he kilwa ndo wakazika!
Mguu mmoja uko Tanzania ..halafu mguu mwingine uko Congo halafu maji ya kunywa aombe?Badala ya kuchota Kwenye mto Congo au mito yeyote ile?
Halafu apite kijijini Kilwa watu wafukuze?Huku huyo mtu ni mkubwa mguu mmoja uko Congo?
 
Mguu mmoja uko Tanzania ..halafu mguu mwingine uko Congo halafu maji ya kunywa aombe?Badala ya kuchota Kwenye mto Congo au mito yeyote ile?
Halafu apite kijijini Kilwa watu wafukuze?Huku huyo mtu ni mkubwa mguu mmoja uko Congo?
... Halafu akinyosha mkono analikaribia Jua; millions of kilometers. Wakati dunia focus ni high-tech sisi bado tupo kwenye masimulizi ya babu kwa wajukuu jamvini.
 
Dogo, hii ni Chai!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…