Mjue binadamu wa ajabu anaitwa Unju bin Unuk

Chai
 
Mguu mmoja uko Tanzania ..halafu mguu mwingine uko Congo halafu maji ya kunywa aombe?Badala ya kuchota Kwenye mto Congo au mito yeyote ile?

Halafu apite kijijini Kilwa watu wafukuze? Huku huyo mtu ni mkubwa mguu mmoja uko Congo?
Mguu mmoja uko Tanzania halafu mwingine uko Congo, sasa akiinama kuomba hayo maji, I bet kifua chake kitakuwa Juba - South Sudan!
 
Pengine Kim Jong Un, huyo nimemsikia sana.
 
Unju bin Unuq (pia: Unju bin Unuku, Unzi Bin Ununuk) ni jina la jitu katika masimulizi ya wakazi wa pwani ya Tanzania. Hadithi zake zasimuliwa kuanzia Bagamoyo hadi Kilwa.

Historia yake inapatikana katika makumbusho ya Kaole huko Bagamoyo.

Moja ya mambo ya ajabu ya mtu huyu ni urefu wake yaani kimo, inasadikiwa alikuwa na urefu mkubwa ulioweza kumfanya atembee baharini na miguu yake kugusa chini.

Pia alikuwa akitembea kutoka nchi hadi nchi kutokana na urefu wake. Inasimuliwa kuwa mmoja kati ya nyayo zake unapatikana kwenye jiwe alilokanyaga huko Tabora, Tanzania, wayo wa mguu wa kushoto wakati wayo wa mguu wa kulia ulionekana kwenye jiwe alilokanyaga huko Kongo.

Inasimuliwa pia akitaka kula alikuwa akichukua samaki baharini kwa mkono na kuchoma katika jua kisha anakula.

Kuhusu maisha yake inasimuliwa kuwa Unju bin Unuk hakuoa wala kuolewa kutokana na umbo lake.

Sehemu nyingine ya hadithi yake ni alipokufa Unju bin Unuq, aligawanyika vipandevipande kutokana na urefu wake na inasemekana kidole chake chenye urefu wa kilometa moja kasoro ndicho kilichopatikana na kuzikwa pale Bagamoyo, lakini hakuna simulizi mwili wake uliobaki uliangukia wapi.

Unju bin Unuq alikuwa na ndugu yake aliyejulikana kama Geofrey bin Unuk, huyu alipatikana maeneo ya Dodoma. Au kwamba Unuq baada ya kupotea kwa muda wa miaka mingi ndugu zake wa mbali sana wameonekana katika mkoa wa Dodoma.
 

Asili ya jina la Unju bin Unuq katika Uarabuni na Biblia​

Jina lake linatokana na Kiarabu cUdj bin Unuq / ‘Anaq عوج بن عنق anayejulikana katika visa vya nchi nyingi za Uislamu kama jitu kubwa sana. Waislamu walipokea hadithi kutoka kwa Wayahudi anakojulikana kwa jina la Og עוֹג‬.

Asili kabisa ni taarifa za Biblia kuhusu mapigano kati ya Wanaisraeli waliotoka Misri na Ogu mfalme wa Bashani (Hesabu 21,33)[1]; Wanaisraeli walimshinda wakiongozwa na Musa.

Ogu alisemekana kuwa mtu mrefu; Kumbukumbu la Torati 3,11 kinamtaja hivi: "aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu".

Katika masimulizi ya Wayahudi sifa hiyo iliendelea kuongezeka; katika Kitabu cha Amosi 2,9 anatajwa (bila kusema jina) kama "Mwamori" "nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni".

Wataalamu Wayahudi wa baadaye waliona ya kwamba vipimo vya Kumb. 3 kuhusu kitanda chake chenye urefu wa mikono yaani dhiraa 10, sawa na mita 4-5, vilihusu mkono wa hilo jitu lenyewe, hivyo walimwona mkubwa zaidi tena.

Kwenye kitabu Berakhot cha Talmudi Ogu anasimuliwa ya kwamba aliweza kuinua mlima aliotaka kurusha dhidi ya Wanaisraeli, lakini Mungu alimzuia[2]. Katika kitabu cha Nidah katika Talmudi Ogu anasemekana ni mtu aliyeishi kabla ya gharika ya Nuhu akiwa ni mmoja wa hao ambao walitunzwa.[3]

Katika Uislamu​

Masimulizi ya Kiyahudi yalipokewa na Waislamu na kupanuliwa tena. Ushahidi uko kwa Al Tabari aliyeandika ya kwamba maiti ya cUdj ilikuwa kama daraja juu ya mto Naili.

Al-Tha'labi aliandika ya kwamba Udj alikuwa na urefu wa dhiraa 23,333 akiweza kunywa kwenye mawingu, kushika ngumi baharini na kuichoma kwenye Jua. Alitembea mbele ya Nuhu wakati wa gharika kuu lakini maji yalifikia magoti yake tu. Aliishi miaka 36,000. Alipoona kambi la Wanaisraeli na Musa alivunja mlima akashika kipande cha kuangamiza kambi lote kwa pigo moja, lakini Mungu alituma ndege waliokula shimo katikati ya mlima uliomuangukia na kumfunga katikati. Hivi Musa aliweza kumshinda kirahisi.[4]

Chanzo: Unju bin Unuq - Wikipedia, kamusi elezo huru

Marejeo

*ʿŪd̲j̲ — Brill Makala UDJdj B. 'ANAK au ANAK,THE ENCYCLOPAEDIA OF ISLAM, NEW EDITION, VOLUME X, T — U, LEIDEN BRILL 2000 uk 777
*OG - JewishEncyclopedia.com Makala OG, katika Jewish Encyclopedia (1906)
 
Ikiwa Mwenyezi Mungu ameelezea kuwa Mwenyezi Mungu hajaacha kafiri hata mmoja duniani, basi ni vipi watafsiri wengine wanaweza kusema kwamba baadhi ya Auj bin Unuq walimwita Ibn Inaq, aliishi tangu wakati wa Noa hadi wakati wa Nabii Musa, walimwita makafiri, holela, kudharauliwa, na kuasi. Wanaiita pia uzushi, hata kuzaliwa na mama wa mmoja wa watoto wa Adamu kutokana na uzinzi. Yeye hula samaki kila wakati ambaye huchukua kutoka baharini, kisha huiteketeza chini ya jua kali hadi mwili wake uwe mrefu.

Aliwahi kumwambia Nuhu akiwa ndani ya safina, "Una sahani gani hapa?" kwa sauti ya dharau. Wanataja, urefu wa Ibn Anaq ulifikia dhiraa 333, na maneno mengine ya kutatanisha, ambayo ikiwa hayakuorodheshwa katika vitabu vingi vya ufafanuzi, historia na vita, kwa kweli hatungehitaji kuijadili, kwa sababu hadithi kama hizi hazina faida na dhaifu, pamoja na kupingana na hoja na naqli.

Hoja ya busara; ni vipi Mwenyezi Mungu angemwangamiza mwana wa Nuhu kwa kutotii, ingawa baba yake alikuwa nabii wa watu na kiongozi wa waumini, wakati Mwenyezi Mungu hakumwangamiza Auj bin Unuq au bin Anaq ingawaje alikuwa jeuri zaidi na holela kama ilivyotajwa ?!

Je! Kwanini Mwenyezi Mungu huwa hana rehema kwa yeyote yule ambaye haamini, hata mama wa mtoto wakati Mwenyezi Mungu anamruhusu shetani katili, dhalimu, mbaya, kafiri sana, na mwasi kama wasemavyo ?!

Chanzo: Kisah Nabi Nuh (Bagian Ke-7) : Mitos Tentang Auj bin Unuq - Syahida.com
 
Hao walikuwa offsprings wa watchers and binti za wanadamu (Mwanzo 6:1-4) known as Nephilim in Hebrew or Anunakis-wana wa anaki in Aramaic/kiaramu.......many lived in antedelluvian world-preflood world (gharika)....walifikia mpaka urefu wa futi 300. Read the book of Enoch and other forgotten/lost books of the Bible.
 
Ni kweli alishawai kuwepo, ispokua hzo sifa zingine umeongeza chuvi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…