Mjue Bodigadi wa Diamond, kumbe ni 'Komandoo Kipensi'

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,093
Reaction score
7,229
Bodigadi wa Diamond, Mwarabu Seleman Mirundi, akifanya mazoezi ya kikomandoo kwenye msitu wa chuo kikuu kuhofia watu wasione mazoezi yake.

Juu picha za wanajeshi wa Irani ambao pia ni makomandoo ambao awefanyanao mazoezi. Hapa akiwajibika kumlinda boss wake nchini Burundi.

Mwarabu Seleman Mirundi akiwa nchini Iran hivi karibuni alipokwenda kwa mara ya kwanza kushiriki michezo ya mapigano ya hatari ambayo hufanywa na wanajeshi hasa walifuvu ukomandoo.

Mwarabu Seleman Mirundi akiwa nyuma ya bendera ya Tanzania tayari kupambana na Komandoo wa Iran ambae hata hivyo alimchakaza vibaya na kuokolewa raundi ya kwanza.

Hiki ni cheti alichotunukiwa nchini Iraq baada ya kumsambaratisha Komandoo wa nchi hiyo ambae hakumtaja jina. Hiki pia cheti alichotunukiwa na nchini Mozambique baada ya kuwatandika wanajeshi kadhaa nchini humo.

Maskani Bongo Tz, Mwarabu akifanya mazoezi mepesi na mmoja wa maofisa usalama wa nchini Tanzania .

Jamaa huyu hakuwa anafahamika sana hata kwenye matamasha mbalimbali ulikuwa huwezi kumkuta lakini baada ya kupata kazi ya kumlinda staa wa Bongo Flava nchini, Naseeb Abdul Diamond, alianza kujulikana zaidi huku watu wakimchukulia kama mtu wa kawaida sana kama mabaunsa wengine.

Jina lake halisi anaitwa Mwarabu Suleiman Mirundi. Baada ya kupata taarifa za kuwa huyu jamaa si mtu wa kawaida kwenye jamii, ilifanyika jitihada za kumtafuta huku kupatikana kwake huwa ni kwa nadra sana. Huwezi kumkuta mitaani kama tuwaonavyo mabaunsa wengine wanazurura mitaani.

Baada ya kutonywa sehemu anapoweza kupatikana kijana huyo ambapo ni msitu wa chuo kikuu ndiko anakofanyia mazoezi mara nyingi akiwa na mwanamuziki na bondia Zola D ndipo nilipofunga safari hadi huko na kumkuta kijana huyo akifanya mazoezi ya hatari kuyaona.

Mwarabu alianza kuelezea ingawa hakupenda watu wajue kama yeye ni mtu wa aina hiyo lakini alianza kufunguka kama ifuatavyo;

"Dada mimi ni Komandoo lakini sio wa JWTZ hapana nimefuvu mazoezi haya ya mapigano nchini Iran toka mwaka 2010 baada ya kwenda kule kucheza mchezo wa kutumia mabavu ndipo niliposhinda kwa kumchakaza vibaya Komandoo wa Iran"

Alisema Mwarabu Baada ya hapo Jeshi la nchi hiyo baada ya kumuona sio mtu wa kawaida kuwa raia wa kawaida ndipo alipochukuliwa Kambini humo kwa ajili ya kufanya mazoezi hayo ya hatari duniani hadi mwaka juzi 2013 ndipo walipompatia cheti cha kuhitimu kama kinavyoonekana pichani.

Hata hivyo Mwarabu anasema kwa jinsi alivyo na mazoezi aliyoyapata chini ya watu kumi hatakiwi kupigana nao hata wakija na shoka isipokuwa zaidi ya hapo ndipo kidogo atawapiga makofi tu na kuwaacha lakini sio aseme atoe kichapo kwani pigo lake moja mtu anabadilishwa jina mara moja na kuitwa marehemu.

Mwarabu ambae kwa sasa ameajiriwa na mwanamuziki Diamond na analipwa mshahara mnono kwa kazi ya kumlinda ambapo hadi sasa amenunua viwanja kadhaa na ujenzi unaendelea na si nyumba za kitoto huku akiwa na usafari zaidi ya gari tatu ambapo moja boss wake alimnunulia na mbili amenunua kwa mshahara anaomlipa na hadi sasa anakafikisha kilo 190 wastani wa kilo 200.




 

Attachments

  • LIVINGSTONE MKOI (3).jpg
    23.8 KB · Views: 1,116
mweupe sana na hana lolote kuna bodigad wa dully alipewa promo humu baadae akaja gundulia analiwa kiboga eti walimuita ngumi jiwe huku anapumuliwa tz kwa mizaha

Alipumuliwa sio kwa kupenda, sijui alifanya msala gani wahuni wakakusanyana wakamfanyia kitu mbaya
 
mweupe sana na hana lolote kuna bodigad wa dully alipewa promo humu baadae akaja gundulia analiwa kiboga eti walimuita ngumi jiwe huku anapumuliwa tz kwa mizaha

Kwa maana hiyo kama bodyguard wa Dully alipumuliwa basi moja kwa moja na huyu anapumuliwa? Kwani huyo ngumi jiwe ni mwalimu wa Mwarabu Fighter?


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…